Kamwelwe aomba matrilioni kugharamia ujenzi, uchukuzi Tanzania

May 4, 2020 4:56 pm · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na mawasiliano yapendekeza bajeti ya Sh4.78 trilioni huku theluthi mbili zikielekezwa uchukuzi. 
  • Imeshuka kutoka Sh4.96 trilioni iliyotengwa mwaka huu wa 2019/2020.
  • Baadhi ya miradi itakayotekelezwa ni ujenzi wa meli, barabara, reli ya kisasa na ununuzi wa ndege tatu. 

Dar es Salaam. Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imeliomba Bunge kuidhinisha Sh4.78 trilioni kwa ajili ya bajeti yake ya mwaka 2020/2021 ambayo theluthi mbili ya fedha hizo zimeelekezwa katika sekta ya uchukuzi. 

Hata hivyo, bajeti hiyo  imeshuka kidogo ikilinganishwa na mwaka huu wa fedha wa 2019/2020 unaoisha Juni 30, 2020 ambapo wizara hiyo ilitengewa Sh4.96 trilioni. 

Waziri wa wizara hiyo, Mhandisi Isack Kamwelwe aliyekuwa akiwasilisha bajeti hiyo leo (Mei 4, 2020) Bungeni jijini Dodoma amesema fedha hizo zitagawanywa katika mafungu matatu ya utekelezaji wa shughuli za wizara hiyo mtambuka. 

Kati ya fedha hizo, Sh1.6 trilioni ni kwa ajili ya sekta ya ujenzi, mawasiliano (Sh15.6 bilioni) na uchukuzi ni Sh3.15 trilioni.

Sekta ya uchukuzi ambayo imetengewa takriban asilimia 66 au theluthi mbili ya bajeti yote ya wizara hiyo katika mwaka ujao, inatarajia kutumia Sh3.1 trilioni ya fedha zake katika miradi ya maendeleo.

“Kati ya fedha hizo, Sh2.9 trilioni ni fedha za ndani na Sh124.5 bilioni ni fedha za nje,” amesema Kamwelwe katika hotuba yake. 


Soma zaidi: 


Miradi itakayofanywa sekta ya uchukuzi

Fedha hizo zitatumika kutekeleza miradi mbalimbali ya usafiri wa majini na nchi kavu ikiwemo ujenzi na ukarabati wa meli zinazotumiwa katika Ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika na Ziwa Nyasa ili kuwarahishia wananchi usafiri. 

Waziri Kamwele amesema wametenga Sh13 bilioni ili kuwezesha uendeshaji na uwekaji wa miundombinu katika jengo la tatu la abiria (TB III) lililo katika Kiwanja cha Ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA). 

“Fedha hizi zitatumika kwa ajili ya kugharamia umeme, maji, vifaa vya zimamoto, viyoyozi, madaraja ya ndege, daraja la abiria, vyoo, maegesho, huduma za mtandao, kuboresha mazingira ya nje ya jengo la abiria, kamera na kituo cha wasindikizaji,” amesema waziri huyo. 

Mfuko wa Reli (Railway Fund) umetengewa Sh289 bilioni ili kugharamia ukarabati wa miundombinu ya reli iliyopo, kujenga reli mpya ya kisasa (Standard Gauge), ukarabati wa vitendea kazi na kugharamia stadi mbalimbali kwa ajili ya miradi ya ujenzi wa reli. 

Katika kuimarisha sekta ya usafiri wa anga, Kamwelwe amesema mwaka 2020/2021 wanakusudia kulipa malipo ya awali ya ununuzi wa ndege mbili mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner na kulipa malipo ya awali ya ununuzi wa ndege moja ya mizigo (freighter) aina ya Boeing 767-300.

Amesema ndege hiyo ya mizigo itasaidia kuongeza mnyororo wa thamani katika bidhaa zetu ikiwemo maua, samaki na bidhaa zitokanazo na samaki, nyama, korosho, matunda na mboga mboga.

Sehemu kubwa ya bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano itaelekezwa katika uboreshaji wa miundombinu ya usafiri. Picha|Mtandao.

Wanawake wakumbukwa

Ili kuongeza ushiriki wa wanawake katika kazi za ujenzi, wizara hiyo imepanga kutoa mafunzo kwa makandarasi wanawake ya namna ya kuomba zabuni na kujaza zabuni kwa usahihi.

Pia watatoa mafunzo kwa wanawake na vikundi vya wanawake juu ya kufanya matengenezo na ukarabati wa barabara kwa kutumia teknolojia ya nguvu kazi na kuwasaidia kusajili kampuni zao za ujenzi. 

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Moshi Kakoso ameliambia Bunge kuwa bajeti hiyo ni nzuri kuboresha miundombinu nchini lakini inahitaji kuongeza kasi ya utekelezaji wake ili kuwawezesha wananchi huduma bora za usafiri.

Amesema wizara hiyo haina budi kuimarisha nguvukazi yake katika masharika na taasisi zake ikiwemo kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) ili kuhakikisha wanasaidia kuongeza mapato kwa Serikali.

“Tunaisihi sana Serikali kuweka mikakati ya kuhakikisha marubani wetu hawachukuliwi na mashirika yenye nguvu kama Emirates,” amesema Kakoso wakati akitoa mapendekezo ya kamati yake.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Unaweza kusema ni maumivu juu ya maumivu kwa watumiaji wa vyombo vya moto vinavyotumia mafuta ya

Unaweza kusema ni maumivu juu ya maumivu kwa watumiaji wa vyombo vya moto vinavyotumia mafuta ya

Nukta TV

Neema Mohamed, Mkurugenzi wa Bone and Blood Foundation, ni shujaa wa ugonjwa wa selimundu Sickl

Neema Mohamed, Mkurugenzi wa Bone and Blood Foundation, ni shujaa wa ugonjwa wa selimundu Sickl

Nukta TV

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ametua kwenye ardhi ya Urusi kwa ziara ya kitaifa ya siku

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ametua kwenye ardhi ya Urusi kwa ziara ya kitaifa ya siku

Nukta TV