Wafanyabiashara wa mchele tabasamu tupu Njombe

May 11, 2020 2:28 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Bei ya jumla ya zao hilo ni zaidi ya mara mbili ya inayotumika Shinyanga, Tabora, Dar es Salaam na mji wa Mpanda ambayo ni Sh100,000. 
  • Wafanyabiashara wa Njombe wanauza maharage kwa Sh250,000 bei ya jumla.

Dar es Salaam. Wafanyabiashara wa mchele katika Mkoa wa Njombe leo watalala na tabasamu baada ya bei ya jumla inayotumika kuuza za hilo kuwa zaidi ya mara mbili ya ile ya mikoa ya Shinyanga, Tabora, Dar es Salaam na mji wa Mpanda. 

Mchele ni miongoni mwa mazao makuu ya chakula yanayotegemewa na Watanzania kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwemo chakula. 

Takwimu za mazao makuu ya chakula zilizotolewa na Wizara ya Viwanda na Biashara leo (Mei 11, 2020) zinaonyesha kuwa gunia la kilo 100 la mchele linauzwa kwa Sh250,000 Njombe, jambo linalofaidisha zaidi wafanyabiashara na wakulima wanaouza zao hilo katika mkoa huo.  

Bei hiyo ya jumla ni mara mbili zaidi ya ile ya Sh100,000 inayotumika katika mikoa ya Shinyanga, Tabora, Dar es Salaam na mji wa Mpanda. 

Hata hivyo, bei inayotumika Njombe ndiyo bei ya juu kabisa ya zao hilo nchini ikilinganishwa na mikoa mingine huku inayotumika Shinyanga, Tabora, Dar es Salaam na mji wa Mpanda ndiyo bei ya chini kabisa. 

Bei ya juu ya leo imepanda kidogo ikilinganishwa na ya Ijumaa Mei 8 iliyorekodiwa katika Mkoa wa Lindi ambapo gunia la kilo 100 la maharage lilikuwa linauzwa kwa Sh 246,000. 

Kwa mujibu wa wizara hiyo, ijumaa kulikuwa hakuna takwimu za mazao za Mkoa wa Njombe. 

Bei ya chini imebaki kama ilivyokuwa Ijumaa isipokuwa imeongezeka mikoa miwili ya Dar es Salaam na Tabora na mji wa Mpanda ambayo inatumia bei hiyo.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
16 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
16 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Nukta TV

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Nukta TV