Trump hajawahi kuripotiwa kuwa na Corona

May 24, 2020 1:02 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Katika video ya uzushi wameweka neno “Rais Trump” na kutoa  neno  “Valet” ambalo ndiyo neno sahihi.
  • Video hiyo ya uzushi ya sekunde 11 imesambaa ulimwenguni kote ikiwemo Tanzania.

Dar es Salaam. Kasi ya kutengeneza na kusambaa kwa habari za uzushi inaongezeka kwa kasi na safari hii kumekuwepo uzushi mwingine ukidai Rais Trump ana corona.

Habari hiyo ambayo ipo katika video ikiwa katika lugha ya Kiingereza inasema “Trump test postive for Covid-19” (Trump akutwa na maambukizi ya Covid-19) na ikidaiwa kuwa habari hiyo imeshawahi  kurushwa na chombo cha Habari cha Fox News cha nchini Marekani.

Video hiyo ya sekunde 11 iliyosambaa ulimwenguni kote kupitia mitandao mbalimbali ya kijami  ikiwemo Tanzania kwenye makundi  ya WhatsApp.

Katika kipande hicho cha video mwandishi wa habari anasikika kwa lugha ya Kiingereza akisema  “Brought to you just a moment ago, Fox News alert …..the White House medical team confirming President Trump has confirmed positive for the coronavirus.”

Katika lugha ya Kiswahili ikiwa na maana; “Habari zilizotufikia hivi punde …. kutoka katika jopo la madaktari katika Ikulu ya White House  zimethibitisha kuwa  Rais Trump ame ambukizwa ugonjwa wa covid-19.”

Kimsingi habari hiyo siyo ya kweli bali ni uzushi.


Zinazohusiana: Ni uzushi mtupu: Wakenya hawajaandamana kupinga zuio la kutotoka nje


Ukweli ni upi?

Video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii siyo ya kweli  kuwa Rais Trump amekutwa na ugonjwa wa Covid-19  bali imehaririwa kwa minajili maalum ya kupotosha (editing) kutoka katika taarifa sahihi  iliyo ripotiwa na  chombo cha habari cha Fox News Mei 7, 2020 inayosema kuwa “Trump valet tests positive for COVID-19”( Msaidizi wa Trump akutwa na covid-19)

Video ya kweli kuhusu habari hiyo inasomeka : “White House medical team confirmed that valet for President Trump has tested positive for COVID-19. The President and Vice President have since been tested and results were negative.”

Katika tafsri ya Kiswahili  timu ya matibabu ya White House imethibitisha kwamba msaidizi wa Rais Trump amepimwa na kukutwa na virusi vya COVID-19. Rais na Makamu wa Rais  walipimwa ila hawakukutwa na maabukizi ya Covid-19.

Katika video ya uzushi wameweka neno “Rais Trump” na kuondoa neno “Valet” ambalo ndiyo neno sahihi.

Pia wamebadilisha maandishi  sahihi yaliyokuwa yanapita  chini ya mkanda ambayo ni“TRUMP VALET TEST POSITIVE FOR COVID-19” na wametoa neno “Valet”na kuweka Trump hivyo video hiyo ya uzushi maneno yanasomeka  “TRUMP TEST POSITIVE FOR COVID-19”.

Lakini mwisho kabisa wa video hiyo ya uzushi wamesahahu  kubadilisha tena kwenye mkanda unaotembea badala ya kuweka  “TRUMP TEST POSITIVE FOR COVID-19” wakaacha maandishi “TRUMP VALET TEST POSITIVE FOR COVID-19”jambo linalo onyesha kuwa ni habari ya kupikwaPicha  ya kwanza kushoto inaonyesha  video ya uzushi  iliyowekwa  neno “Rais Trump”  badala ya neno  “Valet” ambalo ndiyo neno sahihi.IPicha na Mtandao.

Enable Notifications OK No thanks