Watalii waruhusiwa kuingia Italia, Ulaya ikiwaonya raia wake

June 3, 2020 6:50 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Nchi hiyo imefungua milango leo kwa wasafiri kutoka Ulaya kutembelea nchi hiyo.
  • Imesema inataka kuinua tena sekta ya utalii.
  • Baadhi ya nchi za Ulaya zimewaonya raia wake kwenda Italii maana bado Corona haijaisha. 

Italia imefungua milango leo kwa wasafiri kutoka Ulaya kutembelea nchi hiyo baada ya miezi mitatu ya vizuizi vya safari kujinusuru na janga la Corona, kwa matumaini ya kuinua tena sekta ya utalii wakati huu majira ya joto yanapoanza. 

Hata hivyo, bado watalii wana hofu kuingia katika nchi hiyo ambayo bado inakabiliwa na changamoto ya ugonjwa wa virusi vya COVID-19.

Italia ilikuwa nchi ya kwanza kuathiriwa na ugonjwa huo ambapo mpaka sasa imeripoti wagonjwa 233,197 na vifo zaidi ya 33,000.

“Njooni Calabria (mji wa wenye fukwe na milima). Kuna kitisho kimoja tu; wote mtakuwa wanene,” amesema Gavana wa mji huo Jole Santelli wakati akiongea na shirika la habari la CNA kuhusu kuwaruhusu watalii kuingia katika mji huo. 

Bado nchi hiyo inaripoti visa vipya vya Corona kila siku hasa katika mkoa wa Kaskazini wa Lombardy huku wataalam wa afya wakionya kuwa Serikali inapaswa kusubiri kwa muda kabla haijaanza kuwaruhusu wageni kutoka nje ya nchi.


Zinazohusiana


Inatazamiwa kuwa ndege za kimataifa zitaruhusiwa katika majiji matatu tu ya Milan, Rome na Naples na wageni wanaotoka katika nchi za jirani wanaweza kutumia magari, treni na vivuko vya majini kwenda popote kwa ajili ya  mapumziko. 

Tayari Switzerland imewaonya raia wake wanaopanga kwenda Italia kwa sababu wakirudi nyumbani watawajibika kupimwa na kukaa karantini kama inavyopendekezwa. 

Nchi hiyo itafungua mpaka wake na Ujerumani, Ufaransa na Austria Juni 15 lakini siyo na Italia.

Nayo Austria itafungua mpaka wake na Ujerumani, Switzerland, Jamhuri ya Czech, Slovakia na Hungary lakini siyo Italia huku baadhi ya nchi za Ulaya ikiwemo Uingereza, Ubelgiji zimewashauri raia wake wasisafiri kwa sasa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia amezionya nchi hizo za Ulaya ziichukulie nchi yake kama mtu mwenye ukoma kwa sababu imechukua hatua kukabiliana na COVID-19.

Enable Notifications OK No thanks