Utalii wa farasi unavyoweza kubadilisha mtazamo wako wa matembezi

June 18, 2020 12:57 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni kati ya utalii utakaokusogeza karibu zaidi na wanyama pori.
  • Utalii huo ni maarufu nyanda za kaskazini mwa Tanzania na ukanda wa pwani.

Dar es Salaam. Utalii ni zaidi  ya kupanda milima, kuogelea na kufurahia wanyama wa mbugani. Endapo umemaliza kupanda milima yote nchini, umekula vyakula vya kila kabila na umevalia mavazi ya asili ya kila aina vipo vingine vya kuangazia.

Endapo umezoea kumtazama tembo akitetemesha ardhi kwa muondoko wake ukiwa ndani ya gari, unaweza pia kufikiria kufanya hivyo ukiwa juu ya mgongo wa farasi.

Kufanya utalii huo ambao unapatikana nchini katika baadhi ya hifadhi, haihitaji uzoefu mkubwa kwani hautokua peke yako na utapata nafasi ya kujifunza.

Kati ya watoa huduma wa utalii huo ni Kaskazi Horse Safaris ambao wanafanya shughuli za utalii huo kaskazini mwa Tanzania ikiwemo katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.


Zinazohusiana


Wadau wengine wa utalii huo ni Kilimanjaro Tanzanite Safaris ambao pia wanafanya kazi katika mikoa ya Manyara na Arusha.

Kwa mujibu wa huduma kwa wateja wa kampuni hiyo, kufanya utalii huo inakubidi utoboe mfuko kidogo kwani inagharimu Sh207,990 kwa watalii wa ndani na nje ambapo utatalii kwa saa mbili

Unaweza pia kufundishwa jinsi ya kutalii na farasi na “kama wewe ni mzoefu, unaweza kupata muda wa kujumuika na twiga, tembo na swala.”

Sehemu zingine ni pamoja na Zanzibar Horse Club iliyopo visiwani Zanzibar, Makoa Farm iliyopo mkoani Kilimanjaro pamoja na Hifadhi ya Taifa ya Arusha

Unampango gani kitalii mwaka huu? Endelea kusoma habari za nukta kwa kufahamu taarifa juu ya sehemu mbalimbali za kutalii.

Enable Notifications OK No thanks