Ni uzushi: Rais wa Ufaransa hajazuia Waafrika kuingia Ulaya

June 26, 2020 6:21 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Baadhi ya wapotoshaji wamezusha kuwa Waafrika hawaruhusiwi kuingia barani humo mpaka wakubali kupata chanjo ya COVID-19.
  • Habari hiyo siyo ya kweli kwa sababu Macron hajatoa tamko kama hilo. 

Dar es Salaam. Habari za uzushi kuhusu ugonjwa wa virusi vya Corona zinazidi kusambaa kila mahali huku zikiwahusisha hadi viongozi wanaoheshimika duniani.

Safari hii Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amezushiwa kuwa atawazuia raia kutoka bara la Afrika kuingia katika nchi za Ulaya ikiwemo nchi yake kama hawatakubali kupata chanjo ya ugonjwa wa COVID-19.

Habari hiyo iliyoambatana na picha ilichapishwa na tovuti ya wandabiz.com blog  kwa lugha ya kifaransa na na baadaye kutafsiriwa kwa Kiingereza ikiwa na maneno haya “The president of France and colonial master of France Africa says: Any African country that refuses its citizens from taking the Coronavirus vaccine would be banned from travelling in Europe (sic).”

Kwa tafsiri isiyo rasmi habari hiyo inasema “Emmanuel Macron, Rais wa Ufaransa na mkuu  wa wakoloni wa Ufaransa Afrika anasema: Nchi yoyote ya Kiafrika inayokataa raia wake kufanyiwa chanjo ya virusi vya Corona itawekewa marufuku ya kusafairi katika nchi za Ulaya.”

Kimsingi habari hiyo ambayo pia iliwekwa katika mtandao wa Facebook  ni uongo na haina ukweli wowote. 


Zinazohusiana


Ukweli ukoje?

Nukta Fakti imebaini kuwa habari hiyo ambayo imeambatana na picha ya Macron haina ukweli wowote, ni uzushi tu 

Kwanza picha ya Macron iliyotumika katika habari hiyo ilipigwa katika mkutano na wanahabari  Februari 3, 2020 huko Warsa nchini Poland na siyo kama ilivyoelezwa katika habari hiyo. 

Pia Msemaji wa Umoja wa Ulaya nchini Ufaransa Guillaume Roty tayari amekanusha taarifa hiyo alipofanya mahojiano ya Tv5Mode na kubainisha kuwa Rais Macron hajatoa kauli kama hiyo. 

Enable Notifications OK No thanks