Vunja mbavu zako na filamu ya “Hubie Halloween”
- Ni filamu inayofundisha kutokufanya maamuzi kwa kumdharau mtu kwa muonekano wake.
- Inamhusu Hubie ambaye analazimika kufunga safari ya kuokoa mtaa wake.
- Baba huyo ambaye haaminiki kwa lolote na wenzake, analazimika kufanya upelelezi wa kesi ya mauaji iliyotokea mtaani hapo.
Dar es Salaam. Umejiandaaje kuvunjwa mbavu zako kwa burudani? Mchekeshaji wa Marekani, Adam Sandler anaingia ulingoni na filamu ya Hubie Haloween kwa ajili ya kurudisha kicheko chako.
Kama ilivyo kawaida kwa nchi za magharibi, Oktoba 31 kila mwaka watu huadhimisha sikukuu ya Haloween ambapo watu huvalia mavazi mbalimbali yakiwemo ya kutisha ikiwa ni maadhimisho yanayofanyika kufukuza na kujikinga na mizimu.
Hali ndivyo ilivyo kwenye filamu ya Hubie Haloween ambapo Hubie Dubois (Adam Sandler) amekuwa ni mtu anayeandamwa na kila mtu anayetaka kumwekea mtego mtu.
Wakati sikukuu ikikaribia, Dubois ananusa harufu ya mauaji na hivyo kuanza kufuatilia mauaji hayo.
Dubois huyo huyo ambaye amegeuka kuwa kituko mbele ya jamii yake, anawezaje kuaminika kuwa anaongelea jambo la kweli?
Soma Zaidi:
- Daraja la Kigongo Busisi litakavyoinua uchumi kanda ya ziwa
- Unayopaswa kuzingatia kabla ya kununua bidhaa za watoto
- Petroli, mahindi vyachangia kushusha mfumuko wa bei Tanzania
Baada ya kuona kuwa yeye ndiye msaada pekee, anaamua kuvaa viatu na kuanza upelelezi wake.
Atafanikiwa? Ataaminika? Je, upelelezi wake utavumbua ukweli?
Usikose filamu hii iliyoandaliwa chini ya Netflix huku ikiwa bado mpya mtandaoni humo ikiambatana na nyota wachekeshaji kutoka kwenye filamu maarufu kama Grown Ups, Stranger Things, Modern Family na Zoo Keeper.
Latest