Umuhimu wa matangazo ya kidijitali kwa wafanyabiashara

December 3, 2020 6:22 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni pamoja na kumpatia mfanyabiashara takwimu halisi za kiwango cha kusambaa na usomekaji wa tangazo.
  • Pia, humsaidia mfanyabiashara kupata mrejesho juu ya biashara yake kupitia mitandao ya kijamii.
  • Yanatoa fursa ya kufanya uchambuzi juu ya watu waliovutiwa na bidhaa au huduma.

Dar es Salaam. Kama mfanyabiashara unatumia nini kutangaza biashara yako?

Iwe vipeperushi, matangazo ya redio na televisheni, bila shaka lengo lako ni kuwafikia wateja wengi zaidi ili kuikuza biashara yako. 

Wataalam wa masoko wanashauri wafanyabiashara kuwekeza katika matangazo ya kidijitali kwa sababu ni rahisi kupata takwimu halisi za kiwango cha kusambaa kwa tangazo husika.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya masoko ya kidijitali ya Mayocoo, Justice Donatus amesema, kutangaza kidijitali kutakupatia takwimu halisi na hata mrejesho kutoka kwa wateja wako juu ya biashara yako.

“Ukisema uweke tangazo lako barabarani, hauwezi kujua ni wangapi wamesoma, ni wangapi wamechukua hatua ya kutembelea tovuti au mitandao ya kijamii ya kampuni au biashara yako,” amesema Donatus.

Mtaalamu huyo amesema endao mtu akitangaza kidijitali mfano kwa njia ya Instagram, anaweza kuona watu waliofikiwa na tangazo, waliofurahia tangazo hilo na kuchangamana nalo na hata waliochukua hatua ya kutembelea ukurasa wa kampuni ili kujua zaidi kuhusu biashara yako.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

Nukta TV

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Nukta TV

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

Nukta TV

BENEFIT FROM
Nukta ADS
Advertise with us to reach a wider audience with high conversion rates.
Other Nukta Africa Products
Nukta Habari
Stories that matter
Topics
Inuldge yourself with the topics in Nukta
All
Business
Africa
Contact
Tel
+255 750 881 888
Mail
newsroom@nukta.co.tz
Address
Mwananyamala kwa Kopa Dabe House Dar es Salaam TZ, 14108
Social Media

© 2024 Nukta Africa. All Rights Reserved.