Zingatia haya wakati wakupanga sherehe yako

December 18, 2020 4:35 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Hakikisha unafurahia sherehe yako
  • Epuka mikopo isiyo ya lazima
  • Kuwa mbunifu

Dar es Salaam. Unatarajia kuwa na sherehe hivi karibuni? “Baby shower”  Arobaini ya mtoto, Sherehe ya kuaga ukapela, ”Kitchen party” “Send off” ama Harusi? Basi huenda kichwani umejaa mawazo ambayo mara kadhaa yanakukosesha hata usingizi.

Maswali ya “pesa nitatoa wapi”, “je nitafanikiwa”, “vipi ikinyesha mvua” yanaweza kuwa ni kati ya maswali machache yanayo zunguka akilini mwako. 

Zingatia dondoo hizi kwaajili ya kufanya shughuli yako kuwa yenye kumbukumbu nzuri na zaidi, kuwa shughuli uliyoifurahia.

  1. Kabidhi shughuli yako kwa mtaalamu

Mara nyingi unashindwa kufurahia sherehe yako kwasababu umeshikilia kila kitu. Baadhi ya watu huingilia kamati na kutaka kujua kila lililo nyuma ya pazia lakini, hata kamati kwa sasa inakuwa ni masuala yanayopitwa na wakati kwani wapo wataalamu wa sherehe ambao wanaweza kukusaidia kufanya sherehe ambayo ipo kwenye bajeti yako.

“Event planners” ni watu wa kuangazia kipindi cha sheehe yako na kama unaona ni shida kuwapata, unaweza ukachagua hata afikia au mtu unaye mwamini aweze kusimamia kila kitu badala yako kwa kuwa unahitaji kuifurahia siku yako.​Maswali ya “pesa nitatoa wapi”, “je nitafanikiwa”, “vipi ikinyesha mvua” yanaweza kuwa ni kati ya maswali machache yanayo zunguka akilini mwako. Picha| Entrepreneur.com

  1. Weka fedha kwa ajili ya dharura

Kama shughuli yako ina bajeti ya Sh10 milioni, unaweza kuweka hata Sh2 milioni au zaidi kwaajili ya dharula.

Mara nyingine dharura zinaweza kutokea na hivyo kuhitaji kufanya maamuzi magumu na ya haraka.Mfano, sherehe yako inafanyika kwenye bustani na ghafla mvua ikanyesha. Kwa kutumia fedha ya akiba, unaweza kukodi mahema au hata kulipia sehemu kwaajili ya kukamilisha sherehe yako.

  1. Fungamana na bajeti yako

Hakuna haja ya kuingia kwenye mikopo kwaajili ya kuridhisha wageni waalikwa. Mtu anayestahili kuridhika ni wewe. Hivyo, ni vizuri ukafungamana na kiasi cha fedha ulichonacho kwaajili ya kufanya sherehe yako ilihari vitu vya muhimu kama vinywaji, chakula na menginyo yamefikiwa.

Kukopa kwaajili ya sherehe ya masaa machache inaweza kukuumiza kichwa baadaye na hata ulio wafurahisha wasiweze kukusaidia kulipa madeni uliyonayo.


Zinazohusiana


  1. Kuwa mbunifu

Kutokanana sherehe kuwa nyingi, ratiba za sherehe zimekuwa zikifanana. Mathalani kwa harusi, imezoeleka ni kuingia wageni waalikwa, kuingia maharusi, utambulisho, keki na champain chakula, mawaidha kutoka kwa wazazi na kisha mwisho wa sherehe.

Una nafasi ya kuweka sukari kidogo kwenye sherehe yako ili iwe ya tofauti na uifurahie zaidi. Umewahi kuwaza kuwa unaweza kuingia ukumbini kwa namna tofauti? Au kama unaweza kuonda mawaidha na risala na kuweka burudani ili watu washereheke zaidi kwani wageni waalikwa huenda hata hawasikilizi.

  1. Furahia siku yako

Hauna haja ya kuwa na mawazo kiasi cha kusema “bora imeisha” pale sherehe yako ikishapita. Weka kila namna ya kufurahia sherehe yako kwani haitajirudia mara mbili au zaidi.

Unaweza kufikia hatua hii kwa kuzingatia hatua zilizoainishwa hapo juu.

Ni muhimu kufurahia nyakati hizo na uwapendao. Picha| Mtandao

Sherehe ni kitu muhimu kwa mwanadamu. Una kila sababu ya kufurahia mafanikio yako kwani umepitia mengi kuyafanikisha.

Ni muhimu kufurahia nyakati hizo na uwapendao na zaidi kuhakikisha unaifurahia haswa kwani, itakupa ari ya kufanya mambo mengine kwa uweledi ili ushreheke hapo yatakapo fanikiwa.

Nukta Habari (www.nukta.co.tz) inakutakia kila la kheri kwenye sherehe yako.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Nukta TV

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Nukta TV