Wasafi TV yapunguziwa adhabu, kurudi hewani Machi mosi

February 4, 2021 9:06 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetangaza kuipunguzia adhabu televisheni hiyo kutoka kifungo cha miezi sita na itarejea hewani Machi 1.
  • Imepewa masharti matatu ikiwemo kutumikia adhabu yake mpaka tarehe tajwa. 
  • Uamuzi huo unatokana na Wasafi TV kukiri kosa na kuomba kupunguziwa adhabu.

Dar es Salaam. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetangaza kuipunguzia adhabu televisheni ya Wasafi TV kutoka kifungo cha miezi sita na kuiruhusu kuendelea kurusha matangazo yake kuanzia Machi mosi mwaka huu, kwa masharti matatu ikiwemo kutumikia adhabu yake mpaka Februari 28.  

Januari 5 mwaka huu, TCRA ilikifungia kituo hicho  kwa muda wa miezi sita kwa kutangaza maudhui yasiyofaa yaliyokiuka Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta za mwaka 2018.

Kwa mujibu wa mamlaka hiyo, mnamo Januari 1, 2021 majira ya 2:00 hadi saa 5:00 usiku kupitia kipindi cha “Tumewasha Live Concert” Wasafi Tv ilirusha maudhui jongefu yaliyokuwa yakimuonyesha msanii anayejulikana kwa jila la Gift Stanford Joshua Mwakyusa au “Gigy Money” akicheza katika jukwaa katika mitindo iliyokua ikionyesha utupu wa mwili wake. 

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba amesema masharti hayo ni  Wasafi TV kuendelea kutumia adhabu yake mpaka  Februari 28 mwaka huu na baada ya hapo televisheni hiyo itaendelea kurusha matangazo yake.

“Wasafi TV inaelekezwa kuzingatia masharti ya leseni ya kutoa huduma ya maudhui kwa njia ya televisheni,” amesema Kilaba katika taarifa yake aliyoitoa leo Februari 4, 2020. 

Sharti la tatu, Kilaba amesema iwapo Wasafi TV itashindwa, itakataa au kukaidi uamuzi huo, hatua zaidi za kisheria na kiudhibiti zitachukuliwa dhidi ya Wasafi TV. 


Zinazohusiana:


Uamuzi wa kuipunguzia adhabu televisheni hiyo, unatokana televisheni hiyo kuwasilisha maombi TCRA na vielelezo zaidi Januari 21 ikiomba kupitiwa upya kwa adhabu iliyotolewa ya miezi sita. 

“Tarehe 28 Wasafi TV ilifika TCRA kwa ajili ya kusikilizwa maombi hayo,” amesema Kilaba na kubainisha kuwa televisheni hiyo iliwasilisha ushahidi mpya kuonyesha kuwa endapo ushahidi huo ungewasilishwa awali wakati wa usikilizwaji, TCRA ingeweza kutoa adhabu ya kufungiwa miezi sita.

Amesema pia Wasafi TV ilikiri kurusha matangazo mubashara kinyume na leseni yake na kuomba kupunguziwa adhabu yake. 

Baada ya kusikiliza ushahidi wa televisheni hiyo, TCRA imetafakari uamuzi wake wa Januari 5 na sasa itairuhusu televisheni hiyo kuanza tena kurusha matangazo yake Machi mosi baada ya kukamilisha adhabu yake. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV