Guterres: Muziki wa Jazz ni alama ya uhuru, utu

May 1, 2021 7:12 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN) Antonio Guterres  amesema muziki huo ni alama ya utu na uhuru wa mwanadamu.
  • Unaweza kuvuka mipaka iliyowekwa na umaskini na uonevu. 

Dar es Salaam. Licha ya kuwa muziki wa Jazz umekuwa ukitoa burudani kwa watu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN) Antonio Guterres amesema  kuwa mirindimo na miondoko yake inaonyesha utu wa kibinadamu usiyoweza kushindwa na ambao unaweza kuvuka mipaka iliyowekwa na umaskini na uonevu. 

 Mkazo wake wa kuhusu masuala ya usawa, amesema huwapa wanamuziki uhuru wa ubunifu kama watu binafsi wakati wa kufanya matamasha na maonyesho kama sehemu ya sauti ya jamii.

Guterres ametoa ujumbe katika Siku ya kimataifa ya Jazz iliyoadhimishwa huo jana Aprili 30, 2021 huku akieleza kuwa maadhimisho hayo yamekuwa faraja na furaha sio tu kwa kuenzi muziki huo bali kwa uhuru, utofauti wetu na utu wa binadamu.

 “Haya ni maadili ambayo Umoja wa Mataifa unafanya kazi kuyalinda na kuyachagiza duniani kote. Tangu kuzinduliwa kwake muziki wa Jazz umekuwa daraja la kuunganisha wengi na jukumu lake la kihistoria la kupambana na ubaguzi na ubaguzi wa rangi linaendelea kuunganisha tamaduni mbalimbali kote duniani,” amesema Guaterres.


Zinazohusiana:


Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo wa UN, siku hiyo, tunakumbushwa jinsi Jazz inavyoweza kutoa tumaini, uponyaji na nguvu tunapofanya kazi ya kuujenga ulimwengu bora na wenye amani.

Kwa muongo mmoja uliopita, shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni (UNESCO), limekuwa likitangaza ujumbe huu wa siku ya Jazz kote duniani. 

Guterres amehitimisha ujumbe kwake kwa kusema “katika maadhimisho haya ya miaka kumi, hebu tuungane tena kusherehekea ari na maadili ya jazz.” 

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV