Google yawaongezea usalama wanaotafuta vitu mtandaoni

May 25, 2021 10:33 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link

  • Imeongezeka kipengele cha kulinda historia ya vitu unavyotafuta mtandaoni.
  • Kipengele hicho kinazuia mtu mwingine asione historia ya kumbukumbu vitu ulivyotafuta mtandaoni.
  • Huenda ikasaidia kuongeza usalama wa watumiaji wa mtandao wa Google. 

Dar es Salaam. Unapotumia simu yako au kompyuta kuvinjari mtandaoni, unaingia katika tovuti mbalimbali ukitafuta vitu vya aina tofauti tofauti na mara zote, kifaa chako kinahifadhi kumbukumbu ya kote ulikotembelea.

Ikiwa mtu atatumia kompyuta au simu yako ana uwezo wa kuona vitu vyote ambavyo umetafuta katika mtandao wa Google endapo hautofuta historia yako ya kuvinjari. 

Ili kuhakikisha kunakuwa na usiri na faragha wa taarifa za watumiaji wake, Google imeongeza kipenegele kingine katika mtandao wake wa kutafuta vitu mtandaoni ambao unawezesha mtumiaji kuweka neno la siri ambalo halitaruhusu mtu mwingine kuona historia ya vitu ulivyoangalia mtandaoni. 

Ili kuwezesha kipengele hicho katika kifaa chako, unatakiwa kutembelea activity.google.com na bonyeza sehemu ya kudhibiti uthibitisho wa mtumiaji (Manage My Activity verification link) na kisha chagua sehemu ya kuhitaji uthibitishaji wa ziada (Require Extra Verification option).

Baada ya hapo, kisha thibitisha (save) na kisha weka neno siri lako la Google ili kuthibitisha kuwa ni wewe.

Kipengele hiki cha faragha kinasaidia kuficha vitu ulivyotafuta katika mtandao wa Google, historia ya video ulizotazama katika mtandao wa YouTube na maulizo uliyouliza kwa msaidizi wa sauti wa Google (Google Assistant).


Soma zaidi:


Kwa kawaida, historia ya kivinjari chako inaweza isiwe na maana lakini unatakiwa kufahamu kuwa pale inapotazamwa na mtu mwingine, inakuwa ni rahisi mtu kufahamu vitu ambavyo unafanya mtandaoni na kujiweka katika hatari ya kiusalama.

Hiyo inaweza isiwe salama pale simu au kompyuta yako inapodondokea katika mikono mwa mtu usiyemwamini. Inaweza ikawa ni rahisi kudukuliwa katika akaunti zako mbalimbali na hata kutumika vibaya kwa taarifa zako.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW