Rais wa Tanzania ataka benki kuu kujiandaa na ‘Crypto currency’

June 13, 2021 3:31 pm · Nuzulack Dausen
Share
Tweet
Copy Link

Dar es Salaam. Katika kuiandaa Tanzania kufaidika na mapinduzi ya nne ya viwanda, Rais Samia Suluhu Hassan ameigiza Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuanza kujiandaa juu ya namna nchi itakavyotumia teknolojia ya sarafu za mtandaoni maarufu kama ‘Crypto currency’.

Wito huo wa Rais Samia ni moja ya maagizo makubwa kwa kiongozi wa juu zaidi wa Serikali katika kutazamia namna ambavyo teknolojia mpya kama ya blockchain inavyoweza kuingizwa katika mfumo rasmi wa uchumi.

Rais Samia amesema Tehama imeleta Maendeleo makubwa ulimwenguni ambapo miongoni mwa mambo hayo ni kuibuka kwa sarafu mpya zinazotumika mtandaoni za Crypto currency.

Miongoni mwa sarafu mashuhuri za mtandaoni ni Bitcoin ambayo thamani yake imekuwa ikipanda miaka ya hivi karibuni. Sarafu nyingine ni Litecoin, Cardano, Polkadot na Stellar. 

“Najua nchi nyingi duniani hazijazikubali wala kuanza kutumia sarafu hizo. Hata hivyo, wito wangu kwa benki kuu ni vyema mkaanza kufanyia kazi maendeleo hayo, kujitayarisha tu, kukaa tayari. Yakija yakitukamata, yasitukamate hatuko tayari,” amesema Rais Samia wakati akizindua jengo la BoT tawi la Kanda ya Ziwa. 

“Tunaweza tukaona sisi hatuko tayari lakini wananchi wetu wakatutangulia katika hizo ‘system’. Wakaanza kuingia huko katika nchi za nje na wakiingia huko bila shaka yatakuja huku kwetu,” ameongeza.

Mataifa mengi ulimwenguni bado yanasita kuingiza teknolojia ya blockchain na sarafu za mtandaoni katika mifumo rasmi ya kiuchumi. Sarafu za mtandaoni hutumia mfumo wa blockchain. 

Teknolojia ya blockchain ni mfumo wa tehama ambao husaidia kuweka miamala ya biashara kwa uwazi na iwapo umiliki utabadilika au kuongezeka kila mtu aliyepo kwenye mtandao huo huwa ana uwezo kung’amua kilichojiri.

Hivi karibuni El Salvador ilikuwa nchi ya kwanza ulimwenguni kukubali sarafu ya mtandaoni ya Bitcoin kuwa sehemu rasmi ya sarafu katika taifa hilo inayoweza kutumika katika shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Hata hivyo, wachambuzi wa masuala ya fedha na uchumi wameonya kuwa matumizi ya sarafu hizo huenda yakaathiri uchumi kwa kuwa thamani yake hubadilika mara kwa mara jambo linaloweza kuchangia kutokuimalika wa thamani ya biashara mbalimbali.

Licha ya kuwa sarafu za mtandaoni haziruhusiwi Tanzania, baadhi ya wadau wamekuwa wakishawishi mamlaka ziruhusu matumizi ya teknolojia ya blockchain katika shughuli za Serikali ikiwemo kudhibiti ubadhirifu katika mazao na ugavi katika taasisi za umma.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV