Wanafunzi 10 bora matokeo kidato cha sita hawa hapa

July 10, 2021 2:15 pm · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Perucy Astus Mussiba kutoka shule ya Sekondari Canossa ya jijini Dar es Salaam ameongoza kitaifa.
  • Serikali yaingiza wanafunzi sita katika orodha hiyo.
  • Mkoa wa Dar es Salaam watikisa orodha hiyo kwa kuingiza wanafunzi wanne.

Mwanza.  Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya kidato cha sita mwaka 2021 na kutaja wanafunzi 10 bora waliofanya vizuri katika mtihani huo wakiongozwa na Perucy Astus Mussiba kutoka shule ya Sekondari Canossa ya jijini Dar es Salaam.

​Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde akitangaza matokeo hayo leo Jumamosi Julai 10, 2021 visiwani Zanzibar  amesema Perucy aliyeshika nafasi ya kwanza kitaifa alikuwa anachukua mchepua wa PCB (Fizikia, Kemia na Bailojia). 

Nafasi ya pili imechukuliwa na Donald Rulers Mosile kutoka shule ya Sekondari  Kisimiri ya mkoani Arusha huku Cretus Amos Mihayo kutoka Tabora Boys ya Tabora akishika nafasi ya tatu.

Ismail H Mtimwa kutoka Shule ya Sekondari Kibaha ya mkoani Pwani ameshika nafasi ya nne na Olais Julius Molel kutoka shule hiyo hiyo akishika nafasi ya tano.

Nafasi ya sita imeenda kwa Geofrey Sanga wa Tabora boys huku Anorld Andrew Msanga akitawala nafasi ya saba naye kutoka Tabora Boys. 

Caroline Mpale Joune kutoka Canossa ya  jijini Dar es Salaam ameshikilia nafasi ya nane na nafasi ya tisa imeenda kwa John Bugeraha kutoka shule ya sekondari Feza Boys ya jijini Dar es Salaam.

10 bora kitaifa kidato cha sita imefungwa na Herry Mshana wa Feza Boys ya jijini Dar es Salaam.

Katika orodha hiyo ya dhahabu shule za Serikali na binafsi zimechuana vikali ambapo Serikali imeingiza shule sita. Mkoa wa Dar es Salaam umeibuka kidedea katika orodha hiyo baada ya kuingiza wanafunzi wanne ikifuatiwa na Tabora ambayo imeingiza  watatu.

Wasichana hawajafua damu mbele ya wavulana katika orodha hiyo baada ya kufanikiwa kuingia wawili tu.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
25 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
25 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Zungu: Kura zimepigwa , pesa ya Serikali imeruhusiwa kuanza sasa kuitumia

Zungu: Kura zimepigwa , pesa ya Serikali imeruhusiwa kuanza sasa kuitumia

Nukta TV

Bunge la Tanzania lapitisha ya Serikali kwa 97%

Bunge la Tanzania lapitisha ya Serikali kwa 97%

Nukta TV

Hawa hapa wabunge waliopiga kura ya hapana, kupitisha Bajeti ya Serikali

Hawa hapa wabunge waliopiga kura ya hapana, kupitisha Bajeti ya Serikali

Nukta TV