Mikoa mitatu iliyong’ara matokeo kidato cha sita

July 10, 2021 2:56 pm ยท Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Mkoa wa Singida umeshika nafasi ya kwanza kitaifa.
  • Mikoa ya Lindi na Mara imeingia katika orodha hiyo.

Mwanza. Mkoa wa Singida umetajwa kinara katika motokeo ya mtihani wa kidato cha sita kwa mwaka 2021 yaliyotangazwa leo baada ya kushika nafasi ya kwanza kitaifa.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) Dkt. Charles Msonde akitangaza matokeo hayo leo amesema ufaulu wa jumla umepanda kidogo kwa asilimia 0.11 ambapo mwaka 2020 ulikuwa 99.51 na mwaka huu ufaulu ni asilimia 99.62.

Ufaulu huo ni sawa na ongezeko la asilimia 0.11.

Dk Msonde wakati akitangaza matokeo hayo ametaja mikoa mitatu iliyofanya vizuri kuwa ni Singida ambao umeshika nafsi ya kwanza ukifuatiwa na Lindi huku nafasi ya tatu ikienda kwa Mkoa wa Mara.

Singida ambayo ilikuwa na shule 15 idadi ya watahiniwa 1,674 waliofanya mtihani huo, imepata ubora wa ufaulu wa asilimia 73.91 ikiwa ni kiwango cha juu kuliko mikoa mingine.

Licha ya Singida kushika nafasi ya kwanza, haijafanikiwa kuingiza shule wala mwanafunzi katika orodha ya 10 bora kitaifa.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW