Bagamoyo kinara matokeo kidato cha nne mwaka 2020

January 15, 2021 9:47 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo iliyopo mkoa wa Pwani imeshika nafasi ya kwanza kitaifa matokeo ya kidato cha nne 2020.
  • Imefanikiwa kuingiza shule mbili kati ya shule 10 bora kitaifa. 
  • Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Iringa yaingia 10 bora kitaifa. 

Dar es Salaam. Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo iliyopo Mkoa wa Pwani imeshika nafasi ya kwanza kati ya Halmashauri 10 zilizofanya vizuri katika matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka 2020 huku ikifanikiwa kuingiza shule mbili kati ya shule 10 bora kitaifa. 

Katika matokeo hayo yaliyotangazwa leo (Januari 15, 2021) na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) Dk Charles Msonde amezitaja Halmashauri nyingine zilizofanya vizuri kuwa ni Bukoba Mjini ya mkoani Kagera iliyoshika nafasi ya pili. 

​Halmashauri nyingine ni Meru (Arusha), Njombe  (Njombe), Bariadi  (Simiyu), Kibondo (Kigoma), Moshi Manispaa (Kilimanjaro), Kibaha (Pwani), Moshi (Kilimanjaro) na nafasi ya 10 inashikiliwa na Mtwara Mjini ya mkoani Mtwara.

Katika matokeo hayo ya kidato cha nne mikoa ya Pwani na Kilimanjaro imefanikiwa kuingiza Halmshauri mbili kila mmoja.


Soma zaidi: 


Wakati Bagamoyo ikishika nafasi ya kwanza kitaifa, pia imefanikiwa kuingiza shule mbili za Ahmes na Marian Boys katika shule 10 bora kitaifa katika matokeo hayo. 

Katika ngazi ya mkoa, Arusha ndiyo imeongoza kitaifa kwa ufaulu ikifuatiwa na Kilimanjaro ambao umeangushwa kutoka nafasi ya kwanza ulioshika mwaka juzi.

Mkoa mwingine ambao umefanya vizuri katika matokeo hayo ni Iringa ambao ulikua na shule 165 zilizoshiriki mtihani huo.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV