Wawili wanavyovuka vikwazo kujenga penzi lao

August 20, 2021 11:11 am · Herimina
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni filamu inayomhusu mwanadada anayedondoka kwenye penzi na kijana mwenye upofu.
  • Licha ya kuwa mapenzi ni lugha ngeni kwa kijana huyo, taratibu naanza kuielewa.
  • Vikwazo, maneno ya majirani na vicheko kutoka kwa wanaowazunguka havikwamishi kukua kwa penzi hilo.

Dar es Salaam. Je, ni kweli mapungufu ya mtu yanaweza kumfanya mwingine kuvutiwa naye? Basi jibu la swali hilo na mengine mengi utapata katika filamu ya Kikorea ya “Lovers of the Red Sky”.

Filamu/drama hii ni  moja ya drama ambazo zinatarajiwa kutoka mwisho wa mwezi huu, na  jina lake linatokea katika moja ya kitabu kilichoandikwa na mwandishi mashuhuri wa vitabu nchini Korea ya Kusini, Jung Eun-gwol.

Drama ya “Lovers of the Red Sky” au kwa tafsiri ya Kiswahili ni “Wapenzi wa Anga Jekundu”  inaturejesha miaka ya nyuma ya kihistoria ya Korea wakati huo ikiitwa Joseon.

Wakati huo ambao utawala ulikuwa chini ya mamlaka ya kifalme, tunakutana na mwanadada mrembo Hong cheon Ki mwenye uwezo mkubwa wa akili na kipaji cha uchorajI. Uchoraji ukiwa ni kila kitu katika maisha yake.

Wakati maisha yakiendelea bahati inamuangukia binti huyu ambapo chuo cha kifalme cha uchoraji kinachochukua wanaume tu, kinavutiwa na upekee wa kipaji chake, na kinamchagua kuwa mwanamke wa kwanza kuingia katika chuo hicho.

Ni bahati iliyoje? Hata ungekuwa wewe, lazima ungeota mbawa kidogo na kupaa hadi zitakapokupeleka.

Kama jina la drama hii lilivyo, basi siku inafika ambapo Hong anakutana na mwandani wake anayefahamika kama Ha Ram.

Ni siku ambayo jangwa limepata mvua kwani Ha Ram ni kijana mpole na mwenye talanta ya kusoma nyota ambaye amekuwa na maisha ya kujitenga kutokana na hali yake ya upofu.

Hali hiyo aliipata baada ya kuhusika kwenye ajali wakati akiwa mtoto.

Upofu wa Ha Ram haumpiHong kigugumizi cha  kuendeleana leongolake. Picha| CosmoPH.

Penzi jipya kuzaliwa

Ha Ram kutokuwa na marafiki hakuzuii mahaba ya mwanadada Hong ambaye kwa kijana huyo, kama alivyosema Barnaba kwenye kibao chake na Vanessa Mdee cha “siri” , “ treni lake la mapenzi lilikuwa limefunga breki,”.

Kwa slay queens labda wangemkimbia kutokana na ulemavu wake lakini Hong kwake ilikuwa ni zaidi ya mvuto kwani ilimchochea kutaka kuwa naye karibu kiliko kitu au mtu mwingine yeyote.

Mapenzi ni mapya kwa Ha Ram kutokana na hulka yake lakini moyo unajikuta unamkubali binti huyu na kumkaribisha katika maisha yake kama mtu muhimu ambaye hataki kumpoteza.

“Lovers of the Red Sky” imejaa visa mbalimbali vya mapenzi, komedi na mambo ya kihistoria na kwa wapenzi wa filamu za Kikorea basi mwisho wa mwezi huu unasubiriwa kwa hamu sana, kama siku ya kupokea mshahara.

Najua una hamu ya kutaka kujua ni wahusika gani waliopo katika filamu hii, basi katika “Lovers of the Red Sky” tarajia kukutana na mwanadada ambaye anajulikana kwa umashuhuli wa uigizajji wake tangu akiwa mtoto na kwa nchi hiyo anajulikana kama “ Korean little sister”.

Ninamzungumzia Kim Yoo Jung na yawezekana jina likakuchanganya lakini, kama mfuatiliaji wa filamu za Kikorea, hili ni swali kwako.

Unamkumbuka binti mdogo aliyefanya maajabu katika filamu  ya “Sword Fraternity” ya mwaka 2010? Ndiyo huyu huyu Hong ambaye tunamzungumzia kwenye filamu hii.

                      

Jung amekuwa akifanya vizuri katika filamu licha kuwa na umri mdogo, mrembo huyu alizaliwa mwaka 1999 huko Korea ya Kusini na alianza kuwa mwanamitindo akiwa na miaka minne tu.

Wahusika wengine katika filamu hii ni pamoja na Ahn Hyo Seop, Gong Myung na Kwak Si Yang ambao umahiri wao katika uigizaji umewapatia majina makubwa kwenye chati za filamu za Kikorea.

Agosti 28 tuandae macho yetu huko Netflix, TVN, Telegram na SBS kwa ajili ya filamu ya muendelezo ya “Lovers of the Red Sky”.

Mapenzi yakuvuka mito na mabonde, kuvunja minyororo ya tamaduni kwa kufanya kile jamii inakiona ni kosa  ni mbili tatu za Hong katika filamu hii. Unaikosaje?

Gamsahabnida kwa kusikiliza Nukta the podcast

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW