The Squid Game: Filamu iliyoshusha neema Netflix

October 18, 2021 10:53 am · Herimina
Share
Tweet
Copy Link
  • Imeongeza wafuasi milioni 111 wa jukwaa hilo.
  • Imeipatia kampuni hiyo Sh2.1 trilioni.
  • Filamu hiyo ya Kikorea imetazamwa na watu zaidi ya milioni 130.

Dar es salaam. Bila shaka utakuwa umesikia neno ‘The Squid Game’ katika siku za hivi karibuni hasa katika maeneo mbalimbali hasa katika mitandao ya kijamii.

Kama hukusikia basi utakuwa umeitazama filamu hiyo ya nchini Korea kusini, ni filamu ya mwendelezo yenye vipande tisa katika ‘season 1’ .

Hata hivyo, yawezekana unafamu kidogo au hufahamu kabisa mafanikio ya filamu hii na neema iliyoiletea kampuni ya Netflix, ambayo inaonyesha filamu hii.

Licha ya umaarufu wake, filamu hii  imetumia gharama ndogo katika utengenezaji wake, ikiwa ni  Dola za Marekani milioni 21.4 sawa Sh49.4 bilioni.  

Kuifahamu zaidi filamu hii, bonyeza hapa chini 

                     

Netflix ilitangaza filamu hiyo kufanya vizuri zaidi, ambapo watu zaidi ya milioni 130 wameitazama filamu hii katika jukwaa hilo la mtandaoni la kuangalizi filamu duniani. 

Watu hao wametumia zaidi ya saa bilioni 1.4 kuitazama filamu hii, huku ikizishinda  filamu maarufu kama “Lupin”, “Bridgerton” na “The Witcher”.

Mwanzoni mwa mwezi Oktoba, Jarida maarufu la Marekani  la Forbes lilitangaza  The Squid Game kuwa filamu ya kwanza kutazamwa na takriban nchi 90 duniani.

Kufanya vizuri kwa filamu hii, kumewezesha  Netflix kupata mkwanja unokadiriwa kufikia Dola za Marekani milioni 900 (Sh2.1 trilioni) huku hisa za kampuni hiyo zikipanda kwa asilimia saba na kuipa thamani ya kampuni hiyo ikipanda hadi Do  milioni 278.1 (Sh640.9 bilioni) kiwango ambacho kinaendelea kupanda zaidi.

Ni zaidi ya Netflix

Vilevile, filamu hii imesaidia kuongenzeka kwa watumiaji wapya milioni 7.67 wanaojifunza lugha ya Kikorea duniani katika programu tumishi ya Duolingo.

Programu hiyo hutoa fursa kwa watu kujifunza lugha mbalimbali dunia kwa njia rahsi za kimtandao.

The Squid Game ilijipatia umaarufu tangu kutolewa kwake Septemba 17 mwaka huu, huku mpangilio wa visa vyake ukiwavutia zaidi watazamaji na kufanya kuongelewa kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo WhatsApp na hata kutengenezewa vichekesho kama memes.

Ni filamu gani ya Kikorea iliyokuvutia zaidi mwaka huu?

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW