WHO: Mtu aliyepona COVID-19 asimchangie damu mgonjwa anayeugua ugonjwa huo

December 8, 2021 8:53 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni kwa sababu damu hiyo haimsaidii mgonjwa.

Dar es Salaam. Shirika la Afya Duniani (WHO) limewashauri watu waliougua Uviko-19 na kupona kutochangia damu hususan wagonjwa wanaougua ugonjwa huo kwa sababu tafiti zinaonyesha damu hiyo haimsaidii mgonjwa.

​Ushauri huo umetolewa na WHO baada ya jopo lake la kimataifa la wataalamu wa miongozo kuchambua matokeo ya majaribio 16 yaliyohusisha wagonjwa 16,236 ambao wana maambukizi lakini hawako mahututi na wale wagonjwa wa Uviko-19 walio mahututi.

Ingawa hatua za awali za utafiti huo zilionyesha matumaini, lakini utafiti wa sasa  unaonyesha dhahiri kuwa mtu aliyeugua na kupona ugonjwa huo akimuongezea damu mgonjwa anayeugua sasa Uviko-19 haimsaidii kupata nafuu wala kupunguza uhitaji wake wa kuwekwa kwenye mashine ya kusaidia kupumua na zaidi ya yote unaongeza gharama na kuchukua muda mrefu kumuwekea damu mgonjwa. 

WHO imepinga vikali matumizi ya damu kwa mtu aliyeugua na kupona kuwekewa wagonjwa wanaugua sasa wasio mahututi na wale walio mahututi, isipokuwa tuu damu hiyo inaweza kutumika katika muktadha wa kufanya majaribio yaliyodhibitiwa bila mpangilio (RCT). 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
25 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
25 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Lissu alivyotumia saa tisa kujitete mahakamani, aibua hoja tatu nzito

Lissu alivyotumia saa tisa kujitete mahakamani, aibua hoja tatu nzito

Nukta TV

Walimbwende ‘Miss World’, kupewa makabila Tanzania kuwakilisha kimataifa

Walimbwende ‘Miss World’, kupewa makabila Tanzania kuwakilisha kimataifa

Nukta TV

Makonda: Jezi ya Taifa Stars mbaya, hangaikeni  iwe nzuri

Makonda: Jezi ya Taifa Stars mbaya, hangaikeni iwe nzuri

Nukta TV