Njia za asili kudhibiti nzi nyumbani

December 16, 2021 2:37 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni kwa kutumia mimea na mbinu za kufanya usafi.
  • Usitumie sumu kuua panya badala yake tumia mitego ya kunasa.
  • Hakikisha vyombo vyako vya kuhifadhia taka ni visafi na vinafunikwa wakati woote.

Dar es Salaam. Endapo nzi siyo tatizo linalokusumbua mahala pako pa kazi au nyumbani  walau kwa siku hizi za karibuni basi hongera. Kwa wengi, huenda nzi wakawa ni tatizo kubwa ambalo linawaacha kwenye viulizo vya hali yao ya usafi wa nyumbani.

Katika kipindi cha mvua, maji yanaweza kusafirisha vitu mbalimbali ikiwemo taka zinazooza ambazo kwa mujibu wa tovuti ya masuala ya afya, healthline, taka hizo ni kivutio kwa nzi kujazana ili kutaga mayai.

Pamoja na taka za kuoza, kinachovutia nzi kingine ni mbolea na kinyesi cha wanyama hivyo kama wewe ni mfugaji au una wanyama nyumbani, huenda nzi wakawa changamoto kwako.

Hata hivyo, zipo njia za kukabiliana na changamoto hiyo ikiwemo njia asilia na matumizi ya kemikali.

Unawezaje kukabiliana na nzi nyumbani? Panda baadhi ya maua ambayo hufukuza wadudu ikiwemo mbu na nzi au ukatumia dawa ya kuua wadudu.

Hata hivyo, dawa ya dukani huenda ikakugharimu fedha nyingi kwani siyo suluhisho la kudumu. Utumie njia gani nyingine?  Tazama video hii kujifunza.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV