Sehemu za kuwapeleka watoto sikukuu za mwisho wa mwaka

December 26, 2021 5:03 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni pamoja na sehemu za kuogelea.
  • Pia sehemu za chakula wanachokipenda.
  • Unaweza kumkutanisha na rafiki yake ambaye hawajaonana muda mrefu.

Dar es Salaam. Furaha ya watoto huamshwa na vitu vidogo vidogo. Kwa baadhi ya watoto, pipi inatosha kabisa tena ukiambatanisha na chupa ya juisi, basi umeshafanikiwa.

Kwa wengine ni chakula cha tofauti, ice cream na kwa wengine, umtoe mtoko akalione jiji lilivyo.

Kama bado haujafahamu sehemu ya kumpeleka mtoto wako, basi ipo sehemu sahihi. Kama ulikuwa umeshafanya maamuzi, huenda ukabadilisha mawazo baada ya kusoma makala haya.

Sehemu za kuogelea

Ndiyo, ni kipindi cha mwisho wa mwaka na huenda anachohitaji mtoto wako ni kuchezea maji kidogo lakini siyo ya bafuni. 

Kwa ajili ya sikukuu, unaweza kumpeleka sehemu yenye mabwawa ya kuogelea na umwache mtoto wako afurahie maisha.

Hakikisha unakuwa karibu au sehemu hiyo ili kulinda usalama wake.

Kama bajeti yako inaruhusu, unaweza kununua bwawa la plastiki na kuwaruhusu watoto wafurahie nyumbani.

Sehemu ya chakula cha tofauti

Bila shaka pilau, wali, ndizi na viepe ni chakula ambacho hakikosekani kwenye “menu” ya vyakula vya nyumbani. 

Kwenye sikukuu hii, unaweza kumbadilishia mlo mtoto wako kwa kumpeleka sehemu ya chakula. Zipo sehemu nyingi wanazopika vyakula mbalimbali ambavyo anaweza kufurahia.

Ni wewe tu na mfuko wako na kujua chakula pendwa anachokipenda mwanao.


Soma zaidi


Kwa rafiki zake na ndugu

Kama unamjua vyema mtoto wako, basi unamfahamu rafiki yake ambaye anampenda kuliko maelezo.

Huenda ni ndugu na hajamuona kwa muda mrefu. Unaweza kutumia sikukuu hiyo kwenda kuwakutanisha ili na wao wapige stori mbili tatu wakikumbushia kumbukumbu wanazozijua wenyewe.

Wapige picha na muonyeshe baadaye kama sehemu ya ukumbusho wake.

Enable Notifications OK No thanks