Infografia : Mazingira magumu yanavyohatarisha maisha ya wanafunzi Maswa
Dar es Salaam. Wanafunzi 7,788 wa shule za msingi katika Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu wanaishi katika mazingira magumu, jambo linalowaweka katika hatari ya kutozifikia ndoto zao ikiwemo elimu.
Kwa mujibu wa takwimu muhimu za mwaka 2020, katika idadi hiyo, asilimia 94 ambayo ni sawa na wanafunzi 7282 wanatokea katika familia zenye kipato cha chini.Â
Hali hiyo inasababisha wanafunzi hawa kupata kwa shida au kukosa mahitaji muhimu ya shule ikiwemo vitabu vya kujisomea pamoja na madaftari.
​Jambo la hatari zaidi ni kuwa wanafunzi 443 wilayani humo wanaishi au kupita katika maeneo ya wanyamapori, hivyo kuwa hatarini kushambuliwa au kuuwawa na wanyama wakali.
Â
Latest