Mikakati ya kuboresha upatikanaji wa maji Maswa
Dar es Salaam. Katika bajeti ya mwaka 2021/22 Wizara ya Maji ilitenga Sh5.5 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maji ikiwemo vituo 16 vya kuchotea maji katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu.
​Kukamilika kwa miradi hiyo kutawanufaisha wananchi 109,727 wa halmashauri hiyo na hivyo kuwapunguzia tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama yanayohitajika kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo.Â
