Fursa kwa wafugaji wa nyuki mikoa saba Tanzania

February 22, 2022 6:25 am · Herimina
Share
Tweet
Copy Link
  • Serikali yapokea Sh27 bilioni kuendeleza sekta ya nyuki nchini.
  • Fedha hizo zitaekelezwa katika programu ya kuimarisha mifumo ya uzalishaji wa mazao ya nyuki nchini.
  • Zitasaidia kuongezeka thamani ya mazao ya nyuki na kutanua wigo wa masoko ya kimataifa.

Dar es Salaam. Wafugaji wa nyuki katika mikoa saba ya Tanzania ukiwemo Mkoa wa Kigoma wana kila sababu ya kutabasamu kwa sababu siku chache zijazo wanaweza kuongeza uzalishaji wa mazao yao baada ya Serikali kuandaa mpango kabambe kwa ajili yao.

Mazao ya nyuki ni pamoja na asali na nta ambavyo hutumika katika shughuli mbalimbali na hivyo kuwapatia kipato wafugaji.

Hata hivyo, matumizi ya teknolojia duni yamekuwa yakizuia wafugaji wa wadudu hao ambao hutumika kuchavusha maua kutonufaika kikamilifu. 

Kwa kutambua hilo, Serikali ya Tanzania imepokea Sh27 bilioni kupitia programu ya kuwezesha mnyororo wa thamani wa ufugaji nyuki iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).

Programu hiyo itanufaisha wananchi wa mikoa saba ya Tabora, Kigoma, Katavi, Singida, Shinyanga, Mkoa wa Kusini Pemba na Kaskazini Pemba.

Akizindua Programu hiyo  Februari 21 jijini Dodoma, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amesema Serikali inafanya uchambuzi wa kitaalamu kubaini wilaya na vijiji vilivyomo ndani ya mikoa hiyo ambapo mradi huu utatekelezwa.

Programu hiyo itamarisha mifumo ya uzalishaji wa mazao ya nyuki, kuwezesha maeneo ya uchakataji na uongezaji thamani wa mazao ya nyuki katika maeneo husika.

Masanja amesisita ushirikiano kati ya viongozi na wananchi wa mikoa hiyo katika kutekeleza malengo ya programu hiyo.

“Nitumie fursa hii kutoa wito kwa wananchi wote walio katika mikoa husika kushiriki katika kutekeleza programu hii ili iweze kuleta matokeo chanya yanayotarajia,’’ amesema Naibu Waziri Masanja.


Soma zaidi: 


Programu hiyo pia,  itaiwezesha Taasisi ya Utafiti wa Nyuki ipate vitendea kazi katika maabara ya utafiti iliyopo Njiro mkoani Arusha na kuweka mfumo thabiti utakaowezesha ufanyaji wa biashara ya mazao ya nyuki.

Kwa mujibu wa Kitabu Cha Hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2020, tani 30,037 za asali zilizalishwa mwaka juzi ikilinganishwa na tani 30,622 mwaka 2019, sawa na upungufu wa asilimia 1.9. 

Kati ya hizo, tani 2,032.4 zenye thamani ya Sh13.4 bilioni ziliuzwa nje ya nchi ikilinganishwa na tani 607.6 zenye thamani ya Sh4.8 bilioni mwaka 2019. 

Maagizo kwa watendaji

Aidha, naibu waziri huyo amewataka viongozi wa wizara  washirikiane na  Ofisi ya Rais-Tamisemi kutenga maeneo yatakayotangazwa kuwa hifadhi za nyuki ili wananchi na wawekezaji waweze kuyatumia kufuga nyuki kibiashara.

Vilevile, ameelekeza maafisa wa nyuki wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kutoa mafunzo na huduma za ugani kwa wafugaji nyuki walio katika maeneo mbalimbali hapa nchini pamoja na wizara  kuweka mazingira ya kukusanya takwimu za sekta ya ufugaji nyuki.

Balozi wa Ubeliji nchini Tanzania, Peter Van Acker amesema Umoja wa  Ulaya umetoa ufadhili huo ili kuisaidia Tanzania kutumia fursa ya soko la asali lililoko katika nchi za Umoja huo.

” Nchi za Ulaya zinazalisha asali inayotosheleza kwa asilimia 60 ya mahitaji, hivyo ni fursa kwa Tanzania kuchangamkia soko la Ulaya kwenye soko la asilimia 40 hasa ikizingatia Tanzania inashika nafasi ya pili Afrika katika uzalishaji mazao ya nyuki nyuma ya Ethiopia,” amesema Van Acker.

Programu hii itakayotekelezwa kwa miezi 72 inatarajiwa kuwezesha kufanya mapitio ya sera, sheria na kuimarisha mfumo wa udhibiti ubora wa mazao ya nyuki, kuimarisha kiwango cha uzalishaji  wa mazao ya nyuki yenye ubora na kuboresha mifumo ya biashara.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
26 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

Nukta TV

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV