Serikali yatoa tahadhari homa ya manjano

March 9, 2022 12:59 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ugonjwa huo umelipotiwa nchini Kenya.
  • Yawataka wananchi kuchukua tahadhari ugonjwa huo usiingie nchini.
  • Yaimarisha upimaji mipakani na hospitali kuzuia maambukizi.

Dar es Salaam. Waziri wa Afya, Ummy  Mwalimu amewatahadharisha Watanzania kuchukua hatua dhidi ya ugonjwa wa Homa ya manjano ambao umeripotiwa kuwepo nchini Kenya ikiwemo kupata chanjo dhidi ya ugonjwa huo.

Ummy katika taarifa yake iliyotolewa leo Machi 9, 2022, amesema Serikali imepokea taarifa kutoka  Shirika la Afya Duniania (WHO) ya kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa huo nchini Kenya ambao unaweza kuingia nchini.

Kwa mujibu wa Ummy, ugonjwa huo tayari umegharimu maisha ya watu watatu huku watu 15 wakiwa na maambukizi nchini Kenya.

Kutokana na hali hiyo, amewataka Watanzania kuchukua hatua ya kuhakikisha ugonjwa huo hauingii Tanzania kwa sababu mpaka sasa hakuna viashiria vyovyote kuwa ugonjwa huo upo nchini.

“Hapa nchini taarifa ya kipindi cha miezi mitatu iliyopita katika mfumo wa ufuatiliaji wa magonjwa zinaonyesha kuwa hakuna taarifa zinazoashiria kuwepo kwa ugonjwa wa homa ya manjano, pia taarifa za ufuatiliaji wa tetesi za magonjwa haujaashiria kuwepo kwa ugonjwa huo,” amesema.

                         

Hatua ambayo inachukuliwa na Serikali kwa sasa ni kuboresha mifumo ya kutoa vyeti vya kielektroniki vya homa ya manjano mipakani ili kuzuia udanganyifu unaoweza kusababisha kusambaa kwa maambukizi.

“Tutaboresha mifumo ya kutoa vyeti vya kielektroniki vya homa ya manjano mipakani ili kuzuia udanganyifu unaoweza kufanywa na maafisa kuwapa vyeti watu ambao hawajachoma chanjo,” amesema Waziri Mwalimu.

Pamoja na tahadhari hiyo, Waziri Mwalimu ameziagiza hospitali zote za rufaa nchini kuwa na huduma za kupima na kutoa chanjo ya homa ya manjano kwa wasafiri na wenye uhitaji.


Soma zaidi:


Pia amewaagiza maafisa wa afya mipakani kuhakikisha wasafiri wanaoingia kutoka nchi zenye maambukizi wanakua na vyeti vya chanjo dhidi ya ugonjwa huo.

Dalili za ugonjwa wa homa ya manjano kama homa, kuumwa kichwa, maumivu ya misuli na mgongo, mwili kutetemeka, kupoteza hamu ya kula, kichefuchefu na kutapika.

Dalili nyngine ni pamoja na mwili kuwa wa njano pamoja na kutokwa na damu sehemu za wazi.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
25 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
25 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

Nukta TV

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV