Magonjwa ya mfumo wa hewa yalivyowatesa Watanzania mwaka 2022-23

May 15, 2023 11:58 am · admin
Share
Tweet
Copy Link

Dar es Salaam. Watanzania wanatakiwa kuchukua tahadhari ya kujikinga na magonjwa yanayoathiri mfumo wa hewa mara baada ya Takwimu za Wizara ya Afya kubainisha kuwa ugonjwa huo umeathiri watu milioni 7.4 mwaka huu wa fedha.

Ugonjwa huo umeshika namba moja kati ya magonjwa 10 ya wagonjwa wa nje (OPD) yaliyoongoza kwa kuwaathiri Watanzania mwaka 2022/23.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu aliyekuwa akisoma hotuba ya bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka 2023/24, Mei 12, 2023 bungeni jijini Dodoma aliwaambia wabunge kuwa maambukizi katika mfumo wa hewa ndio umeathiri watu wengi zaidi kati ya magonjwa 10 ya nje (OPD).

Ugonjwa huo ulishambulia watu milioni 7.4 sawa na asilimia 24 ya watu milioni 31.4 walioathirika na magonjwa hayo 10.

“Magonjwa yaliyoongoza katika kuwaathiri zaidi wananchi na kuwasababishia kwenda katika vituo vya huduma kupata matibabu ni maambukizi katika mfumo wa hewa asilimia 24, maambukizi ya njia ya mkojo asilimia 13, malaria (asilimia ),” amesema Ummy Mwalimu.

Magonjwa mengine ni Nimonia iliyoathiri watu milioni 1.3, kuhara chini ya siku 14 watu milioni 1.2, shinikizo la damu watu milioni 1.1 yakifuatiwa na magonjwa mengine ya mfumo wa mmeng’enyo , minyoo, vidonda vya tumbo na fangasi. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV