Rais Samia afanya mabadiliko Baraza la Mawaziri

April 1, 2022 4:43 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Amefanya mabadiliko madogo yaliyohusisha wizara tatu.

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri yaliyohusisha wizara tatu kwa mawaziri wake kubadilishiwa majukumu.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus katika taarifa yake iliyotolewa Machi 31, 2022 amesema katika mabadiliko hayo aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, George Simbachawene amehamishiwa Wizara ya Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera na Uratibu.

Nafasi ya Simbachawene imechukuliwa na Dk Damas Ndumbaro, aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii.

Rais Samia amemteua Balozi Dk Pindi Chana kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii akitokea Wizara ya Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera na Uratibu.

Taarifa ya Ikulu imeeleza kuwa mabadiliko hayo yaanza mara moja.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
26 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Lissu: Serikali haikutishwa, hivyo hakuna kosa la uhaini

Lissu: Serikali haikutishwa, hivyo hakuna kosa la uhaini

Nukta TV

Ratiba rasmi mitihani ya darasa la nne, saba na kidato cha pili na nne 2026.

Ratiba rasmi mitihani ya darasa la nne, saba na kidato cha pili na nne 2026.

Nukta TV

Wanu ataja changamoto sita, ratiba ya mitihani ya taifa yabadilika

Wanu ataja changamoto sita, ratiba ya mitihani ya taifa yabadilika

Nukta TV