Profesa Ngowi afariki dunia ajalini Pwani
March 28, 2022 7:05 am ·
Mwandishi
Dar es Salaam. Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Ndaki ya Dar es Salaam, Profesa Honest Ngowi na dereva wake wamepoteza maisha katika ajali ya gari leo asubuhi maeneo ya Mlandizi mkoani Pwani.
Taarifa zinaeleza kuwa wamefariki baada ya gari aina ya Land Cruiser walilokuwa wanasafiria kuangukiwa na lori.
Taarifa zaidi zitakujia, baki nasi.