Ni ushindani: Lexus kuingiza sokoni gari la umeme mwezi huu
Gari mpya ya umeme ya Lexus RZ inayotarajia kuingia sokoni hivi karibuni. Picha| Lexus.
- Inatarajiwa kutoka Aprili 20, 2022.
- Kampuni hiyo ya Japan kuongeza ushindani kwa Tesla.
- Gari hii ni mwanzo wa safari ya lexus kuwa kampuni ya magari ya umeme pekee.
Dar es Salaam. Tumeshasikia kutoka kwa Toyota, Subaru, Apple na Meredes Benz kuhusu ujio wa magari yanayotumia umeme kutoka kampuni hizo za zinazotengeneza magari duniani.
Kampuni ya magari ya Lexus ya nchini Japan imeingia katika ushindani wa kutengeneza magari ya umeme, ikiwa ni hatua ya kuboresha sekta ya usafiri dunia kutumia teknolojia rafiki kwa mazingira.
Kampuni hiyo inayomilikiwa na kampuni mama ya Toyota imetangaza kuitambulisha gari yake ya umeme Jumatano ya Aprili 20 mwaka huu huku picha tangulizi za gari hilo zikionyesha teknolojia zinazoambatana na gari hiyo.
Moja wapo ya teknolojia iliyoonekana ni usukani wa “yoke” ambao huenda Lexus amejifunza kutoka kwa gari za umeme za kampuni ya Tesla.
Soma zaidi:
- Mercedes yaja na mpango wa gari la umeme lenye betri la kilometa 1,000
- Subaru, Toyota kuingiza sokoni magari ya umeme 2022
- Apple kuingiza sokoni gari la umeme 2023
Wakati Toyota ikitangaza gari yake ya BZ4X iliainisha kuwa mtu ana uwezo wa kuchagua gari yake iwe na usukani wa kawaida au Yoke lakini Lexus haijaweka wazi kama mtumiaji atakuwa na uwanja wa kuchagua.
Gari hiyo iliyopewa jina la RZ 450e, huenda ikazinduliwa sambamba na gari nyingine kutoka kwa Lexus ambayo ina muundo sawa na ule wa BZ4X ya Toyota.
Kwa wale wanaojua kilichopo kati ya Toyota Harrier na Lexus Harrier wanaweza kuelewa ninachozungumzia.
Ujio wa gari hiyo ya umeme, ni hatua za Lexus kuachana na magari ya petroli na kujikita katika utengenezaji wa magari ya umeme pekee ifikapo mwaka 2035.
Gari mpya ya umeme ya Lexus itakuja na maajabu yapi? Usikae mbali na ukurasa wa Nukta Habari upate mbivu na mbichi.
Latest