Zingatia haya unapochagua kava la simu yako

May 10, 2022 8:15 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni pamoja na kuchagua kava lililotengenezwa kwa malighafiya ulinzi wa simu.
  • Hakikisha unazingatia matumizi yako ya kilasiku.
  • Usichague kava kwa kuangalia rangi na uzuri, zingatia usalama wa simu zaidi.

Dar es Salaam. Kununua kava siyo tu suala la  kuangalia rangi, uzuri au urembo. Unatakiwa  kuzingatia zaidi usalama wa simu ambayo unalenga kuilinda ili isichubuke, isipasuke  au isiingie vumbi.         

Ili kuwa na uhakika wa kava la simu unalochagua Zingatia yafuatayo

Zingatia malighafi

Unapochagua kava kwa ajili ya simu yako unashauriwa kununua kava iliyotengenezwa kwa malighafi yenye uwezo wa kustahimili mshtuko (shock) hasa pale simu yako inapoanguka kwenye sakafu au mahala pagumu.

Tovuti ya masuala ya teknolojia ya wired.com inashauri kuchagua kava iliyotengenezwa kwa malighafi ya mpira au “silicone”.

Malighafi haya yana uwezo wa kuhimili mshtuko wa simu na kuilinda isipasuke kioo endapo imedondokea upande.

Wembamba, unene

Wapo ambao hawavutiwi na  makava manene kwa sababu yanawakera mfukoni na simu zinaonekana kubwa. Lakini siri iliyopo nyuma ya unene wa kava hizo ni uwezo wa kuilinda simu yako na ajali.

Kwa mtu ambaye anadondosha simu yake mara kwa mara, anashauriwa kununua kava ambalo ni kubwa kidogo ili kuilinda simu yake. Kwa mtu ambaye simu yake hutulia mfukoni na haidondoshi, anaweza kununua kava jembamba ambalo linaendana na muundo wa simu yake.

Hakikisha sehemu ya kamera ya nyuma na mbele inalindwa na kava unalonunua.


Soma zaidi:


Mbembwe

Kava za simu zinakuja na mbembwe nyingi hivyo cha kuzingatia ni kama mbwembe iliyopo kwenye kava yako itakurahisishia matumizi ya simu yako.

Mfano, zipo kava ambazo zina kipete cha kushikilia simu yako wakati  unatazama filamu.

Pia zipo kava ambazo zimeunganishwa na betri kwa ajili ya kuchaji simu. Unaweza kuziita kava za “power bank” hizi zitamfaa mtu ambaye anatumia simu kwa muda mrefu hivyo kuhitaji chaji ya ziada.

Mahitaji na eneo la kazi

Unaponunua kava lako hakikisha unazingatia mahitaji yako pamoja na eneo la kazi. Mfano, tovuti ya wire imeainisha kuwa zipo kava kwa ajili ya kuitumia simu yako hata ndani ya maji na zipo ambazo zinaziba sehemu ambazo maji hayatakiwi kuingia.

Kwa ambao wanaishi kwenye mazingira ya vumbi, zipo pia kava ambazo zinazuia vumbi kuingia kwenye simu yako na kuzuia madhara kwenye kifaa hicho.

Hakikisha unachagua kava huku ukijua mahitaji yako ni yapi.

Usihangaike na rangi, jali usalama wa simu yako kwanza. Picha| Phone Loops.

Hali yako ya usafi

Unawezaje kwenda kununua kava jeupe wakati uanaijua hali yako ya usafi inahitaji maombi?

Pale unapochagua kava, hakikisha unachagua la rangi ambayo inaendana na usafi wako au hali halisi ya matumizi.

Mengine ni pamoja na kuchagua kava ambalo linaendana sawa sawa na simu yako na hakikisha linatoshea vyema. Usichague kava ambalo litabandua kinga yako ya skrini (screen protector) au kava ambalo linaacha simu yako wazi sana.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW