Inang’ata na kupuliza: Bei ya mahindi ikipanda Tanzania

May 12, 2022 7:49 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Imepanda kwa Sh13,033 ndani ya mwaka mmoja uliopita.
  • Mahindi yachangia kupaisha mfumuko wa bei Aprili kwa asilimia 4. mwezi Julai.
  • BoT yasema ongezeko la mahitaji lachangia bei kupanda.

Dar es Salaam. Wakulima na wafanyabiashara huenda wakaendelea kunufaika na kilimo cha mahindi, baada ya bei ya zao hilo kupanda kwa Sh13,033 ndani ya kipindi cha mwaka mmoja uliopita, huku ikiiacha maumivu kwa wanunuzi wa chakula nchini Tanzania. 

Ripoti ya Mapitio ya Uchumi kwa mwezi Aprili 2022 (Monthly Economic Review) iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT)  inaeleza kuwa bei ya jumla ya gunia la kilo 100 la mahindi kwa mwaka unaoishia Machi 2022 ilikuwa Sh60,996 ikipanda kutoka Sh47,963 iliyorekodiwa kipindi kama hicho mwaka jana.

Bei hiyo ya Machi ni sawa na ongezeko la Sh13,033 au sawa na asilimia 27.2.

Kupanda kwa bei ya mahindi kutawafaidisha zaidi wakulima ambao wamewekeza kulima zao hilo ili kujipatia kipato cha kuendesha familia huku wanunuzi wakilazimika kutoboa mifuko yao zaidi kupata zao hilo.

Mahindi ni miongoni mwa mazao makuu ya chakula yanayojumuisha mchele, maharage, viazi mviringo, mahindi, mtama, uwele na ulezi.

BoT katika ripoti hiyo iliyotolewa Mei 11, 2022 imeeleza kuwa katika kipindi hicho, karibu bei za mazao yote ya chakula zilipanda kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya chakula ya ndani na nchi jirani za Afrika Mashariki.

“Kupanda kwa bei ni mwitikio wa kuongezeka kwa mahitaji ya chakula kutoka nchi jirani na mavuno ya mvua za vuli,” imeeleza BoT.

Licha ya bei ya mahindi kupanda kwa mwaka mmoja uliopita, bei za kila mwezi zimekuwa zikishuka kwa miezi miwili mfululizo iliyopita.

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa mwezi Januari mwaka huu bei ya jumla ya mahindi ilikuwa Sh65,864 lakini mwezi uliofuata wa Februari ilishuka hadi Sh62,326 kabla haijashuka zaidi mwezi Machi ambapo ilikuwa Sh60,996.  

Hali hiyo inaweza kuwa imesababishwa na uwepo wa akiba ya kutosha na wakulima kukosa soko la uhakika la mazao yao.


Soma zaidi:


Athari za kupanda bei ya mahindi

Huenda kupanda kwa bei ya mahindi kumechangia kupandisha kiwango cha mfumuko wa bei za bidhaa na huduma nchini kwa mwezi Aprili mwaka huu.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili, 2022 umeongezeka hadi asilimia 3.8 kutoka asilimia 3.6 kwa mwaka ulioishia mwezi Machi, 2022.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili, 2022 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Machi, 2022. 

Mahindi ni miongoni mwa bidhaa zilizochangia kupaisha mfumuko wa bei ambapo NBS imesema yalipanda kwa asilimia 4 mwezi uliopita.

Bidhaa nyingine za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko wa bei ni pamoja na mchele kwa asilimia 0.7, mtama (asilimia 1.5), mahindi (asilimia 4), unga wa ngano (asilimia 7.6), unga wa mtama (asilimia 0.7) na unga wa mahindi kwa asilimia 2.1.

Bei za vyakula zinaweza kuendelea kupanda siku za usoni kutokana na vita ya Ukraine na Urusi na kupanda kwa bei ya mafuta ambayo imesababisha kuongezeka kwa gharama za usafiri na kutatiza mifumo ya masoko ya bidhaa duniani.


Tangazo:


Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
6 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
6 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV