Dar es salaam yaongoza maambukizi ya Uviko-19 Julai

August 27, 2022 10:21 am · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Yachukua zaidi ya theluthi mbili ya maambukizi.
  • Wananchi wahimizwa kupata Chanjo. 

Dar es Salaam. Mkoa wa Dar es salaam umeongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya maambukizi mapya ya ugonjwa wa Uviko-19 nchini Tanzania mwezi uliopita wa Julai.

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Afya kuhusu mwenendo wa ugonjwa wa Uviko-19 iliyotolewa hivi karibuni, imebainisha kuwa kati ya wagonjwa 543 walioripotiwa Julai 2 hadi 29, wagonjwa 366 wametoka Mkoa wa Dar es salaam.

Hiyo ni sawa kusema takriban wagonjwa 7 kati ya 10 walitoka katika mkoa huo.

Kati ya wagonjwa hao 543,  watu 10 walilazwa huku wote wakiwa hawajachanja.

Hadi kufikia Julai 29 mwaka huu,  jumla ya watu 38,201 wamepata maambukizi ya Uviko-19 nchini Tanzania huku 801 wakipoteza maisha.

Wananchi wameaswa kuendelea kuchukua tafadhali kwa kupata chanjo ya Uviko-19, kuvaa barakoa, kuosha mikono kwa sabuni na maji tiririka. 

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW