Zaidi ya Sh22 bilioni kuimarisha afya ya mimea, usalama wa chakula Tanzania

September 27, 2022 5:16 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Zitatolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) kwa kushirikiana na  Muungano wa Ulaya (EU).
  • Zitasaidia kufungua soko la kimataifa kwa bidhaa za Tanzania.
  • Ndege zisizo na rubani kutumika katika mradi huo. 

Katika kutekeleza lengo namba 15 la  Maendeleo  Endelevu (SDGs) kuhusu kuimarisha uhai wa viumbe vya nchi kavu, Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) kwa kushirikiana na  Muungano wa Ulaya (EU) limezindua  mradi wa kuimarisha huduma za afya ya mimea na usalama wa chakula nchini Tanzania.

Afisa Afya ya Mimea kutoka FAO, Mushobozi Baithani amesema lengo la mradi huo ni kuboresha sekta ya mimea na mazao pamoja na kutatua changamoto kwa wafanyabiashara.

“Tanzania wakulima wake wamekuwa wakilima mazao na kusafirisha nje ya nchi lakini zimetokea changamoto kwamba mzigo unafika kule halafu unazuiwa kuingia pengine baada ya kukaguliwa unakutwa na visumbufu, wadudu au umepimwa wamekuta viwango vya viautilifu vilivyowekwa kwenye chakula ni vingi na hakifai kuliwa,” amesema Baithani.


Soma zaidi: 


Amesema mradi huo wa miaka mitatu na  utatumia zaidi ya Dola za Marekani milioni 9 sawa na Sh22 bilioni.

“Umoja wa Ulaya umetoa zaidi ya Dola za Marekani milioni 9 ambazo tutaenda kurekebisha vituo 19 mipakani, tutarekebisha maabara nne, tutanunua vifaaa pamoja na kutengeneza mfumo wa kidigitali utakaotumika kukusanya takwimu mashambani na tumetoa ufadhili wa masomo ya urushaji wa ndege zisizo na rubani kwa wakaguzi 20,” ameongeza Baithani.

Efraim Njau ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa  Mamlaka ya Afya ya Mimea na Udhibiti wa Viuatilifu Tanzania (TPHPA) amesema mradi huo utatusaidia kufungua masoko mapya ya kimataifa ikizingatiwa kuwa utawawezesha wakulima kuzalisha mazao yenye ubora wa hali ya juu. 

“Tutaenda kulima mazao mapya kama soko la maparachihi, maua, pilipili na tangawizi sasa mazao haya yanafuata huu mfumo,” amesema Njau.

Mradi huo pia utatoa mafunzo ya kuendesha ndege zisizo na rubani kwa wakaguzi 20 ili kuwawezesha kufanya tafiti na uchunguzi wa visumbufu kama wadudu na magonjwa yanayoshambulia mazao ya chakula, biashara pamoja na mimea. 

/
No matches found for this filter
31 May, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
31 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
31 May, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

Nukta TV

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

Nukta TV

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

Nukta TV