Majaliwa: Soko zuri ni tumbaku bora

October 19, 2022 7:11 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Amesema soko lipo la kutosha kimataifa.

Dar es Salaam. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema licha ya wakulima kuwekeza katika kilimo cha tumbaku wanatakiwa kuzingatia viwango vya ubora ili zao hilo likubaliwe kwenye soko la kimataifa.

“Serikali yenu inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan haitawatupa mkono, nami kwa maelezo yenu ya leo nitamfikishia salamu Mheshimiwa Rais kuwa mmeazimia mtalima zaidi tumbaku,” amesema.

                     

Ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumanne, Oktoba 18,  2022)  wakati akizungumza na wadau wa zao la tumbaku wilayani Namtumbo Katika Mkoa wa Ruvuma kwenye ukumbi wa shule ya sekondari ya Nasuli, wilayani humo. 

Wadau hao wanajumuisha wakulima, wanunuzi, wenye viwanda, maafisa kilimo, wasambazaji mbolea na wenye mabenki.

 Waziri Mkuu amewapa maagizo viongozi wa mkoa na wilaya wahakikishe kuwa pembejeo za kilimo zinazotolewa na Serikali kwa njia ya ruzuku zinawafikia walengwa na hakuna  ubadhirifu unaofanywa. 

Akitoa maelekezo kwa Bodi ya Tumbaku, Waziri Mkuu ametaka kuwepo na mikakati madhubuti ya kuongeza uzalishaji wa zao hilo ili kufikia malengo yaliyowekwa na kusisitiza kuwa wakulima wa tumbaku waelimishwe kufuata mbinu bora za kilimo ili wazalishe kwa tija.

 “Bodi ya Tumbaku isimamie upatikanaji wa pembejeo na kuhakikisha zinawafikia wakulima kwa wakati. Kwa kuwa msimu wa uzalishaji wa tumbaku umeanza, pembejeo katika zao hilo ziharakishwe kuwafikia wakulima,” amesisitiza.

 Kuhusu malipo kwa wakulima wa zao hilo, Waziri Mkuu ametaka usimamizi wa malipo ya wakulima uimarishwe ili wakulima walipwe kwa wakati. 

“Masoko ya uuzaji wa tumbaku yaimarishwe sambamba na kutatua changamoto zilizopo ili wakulima wa tumbaku wapate tija zaidi,” ameongeza.

/
No matches found for this filter
31 May, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
31 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
31 May, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

Nukta TV

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

Nukta TV

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

Nukta TV