UNICEF: Matibabu ya VVU kwa watoto, vijana yamepungua

November 29, 2022 8:42 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Watoto na Vijana 110,000 walifariki dunia mwaka 2021 kutokana na sababu zinazohusiana na Ukimwi 
  • Watoto na vijana wanajumuisha asilimia 17 ya vifo vyote vilivyohusiana na Ukimwi.

Dar es Salaam. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) limesema matibabu ya Virusi vya Ukimwi (VVU) kwa vijana na watoto yamepungua kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita huku idadi ya maambukizi mapya ikiongezeka.

Kwa mujibu wa ripoti ya UNICEFya masuala ya Ukimwi iliyotolewa Novemba 28, 2022  jijini New York, Marekani inasema upungufu wa matibabu kwa makundi hayo duniani umesababisha vijana na watoto kuanzia umri wa 0 mpaka 19 kupoteza maisha.

“Takribani vijana na watoto 110,000 wa umri wa miaka 0-19 wamekufa kutokana na sababu zinazohusiana na Ukimwi kwa  mwaka 2021,” imesema ripoti  hiyo.

Ripoti hiyo inafafanua zaidi kuwa maambukizi mapya ya VVU kwa  vijana 310,000 yameripotiwa kwa mwaka 2021 na kufanya idadi ya vijana wenye VVU duniani kufikia milioni 2.7.

Licha ya maambukizi hayo  kuchangia asilimia saba tu  ya watu wote wanaoishi na VVU duniani, watoto na vijana wanajumuisha asilimia 17 ya vifo vyote vilivyohusiana na Ukimwi na asilimia 21 ya maambukizi mapya ya VVU kwa  mwaka 2021.  

Anurita Bains, Mwakilishi wa UNICEF kuhusu masuala ya  VVU na Ukimwi anasema hali ya kupungua kwa kwa huduma za ugonjwa huo kwa watoto na vijana ndani ya miaka mitatu iliyopita siyo jambo la kawaida na linaweza kuweka makundi hayo kwenye hatari ya magonjwa na vifo.

 “Watoto wanaathirika vibaya kwa sababu kwa pamoja tunashindwa kuwapata na kuwapima na kuwapatia matibabu ya kuokoa maisha. Kila siku inayopita bila maendeleo, zaidi ya watoto na vijana 300 hupoteza vita vyao dhidi ya Ukimwi.” ameongeza Bains.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa huduma zinazotolewa kwa watu wazima wanaoishi na VVU ni asilimia 76  ambayo ni asilimia 20 zaidi ya huduma wanayopatiwa watoto.  


Soma zaidi


Mapambano dhidi ya VVU,bado kuna matumaini 

Hata hivyo, ripoti hiyo ya UNICEF inaonyesha kuwa mwelekeo wa muda mrefu wa mapambano dhidi ya ugonjwa huo bado ni mzuri.

Maambukizi mapya ya VVU miongoni mwa watoto wadogo  wa umri wa miaka 0-14 yalipungua kwa asilimia 52 kati ya mwaka 2010 hadi 2021, na maambukizi mapya kati ya vijana wa umri wa miaka 15-19 pia yalipungua kwa asilimia 40.  

“Vile vile, matibabu ya kurefusha maisha miongoni mwa wanawake wajawazito wanaoishi na VVU iliongezeka kutoka asilimia 46 hadi asilimia 81 katika muongo mmoja uliopita,” imesema ripoti hiyo.

Riipoti  hiyo inasema kunatokana na sababu mbalimbali  ikiwa ni pamoja na janga la Uviko-19 na majanga mengine ya kimataifa, ambayo yameongeza unyanyapaa na umaskini, lakini pia ni taswira ya utashi wa kisiasa unaofifia na hatua za kukabiliana na ukimwi kwa watoto.  

“Ulimwenguni kote, asilimia ndogo ya watoto wanaoishi na VVU walipata matibabu ambayo ni asilimia 52 ambayo imeongezeka kidogo  sana katika miaka michache iliyopita,” imesema ripoti hiyo.

/
No matches found for this filter
30 May, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
30 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
30 May, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

Nukta TV

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

Nukta TV

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

Nukta TV