Mapato mauzo nje ya nchi yapaa, dhahabu ikishuka kwa asilimia 1.1

December 13, 2022 8:17 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Mapato ya jumla ya mauzo ya nje ya nchi yameongezeka kwa takriban asilimia 23.2.
  • Mapato ya dhahabu yashuka kwa asilimia 1.1 hadi Sh2.81 bilioni.

Dar es Salaam. Mapato yatokanayo na mauzo ya dhahabu nje ya nchi yameshuka kwa asilimia 1.1 ndani ya mwaka mmoja katika mwaka unaoishia Oktoba 2022 ikichangiwa zaidi na kushuka kwa bei ya bidhaa hiyo katika soko la dunia. 

Ripoti ya tathmini ya uchumi ya mwezi Novemba 2022 iliyotolewa hivi karibuni na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inabainisha kuwa mauzo ya dhahabu nje ya nchi yalifikia Dola za Marekani 2.81 bilioni (Sh6.5 trilioni) Oktoba mwaka huu kutoka Dola za Marekani 2.84 bilioni (Sh6.6 trilioni) Oktoba 2021.

“Kupungua kwa mauzo ya dhahabu kumechangiwa na kupungua kwa bei katika soko la dunia,” inasomeka sehemu ya ripoti hiyo.

Licha ya mauzo yake kushuka, dhahabu ni miongoni mwa bidhaa zilizochochea pia ukuaji wa jumla wa mapato yatokanayo na mauzo ya nje ya nchi kwa mwaka ulioshia Oktoba 2022.

Mauzo ya dhahabu, kwa mujibu wa ripoti hiyo, yalikuwa asilimia 39 ya bidhaa zote zilizouzwa nje ya nchi katika mwaka ulioishia Oktoba mwaka huu.

BoT imesema kwa ujumla mapato yatokanayo na mauzo nje ya nchi yalipaa kwa asilimia 23.2 hadi Dola za Marekani 11.8 bilioni (Sh27.6 trilioni) kutoka Dola za Marekani 9.6 bilioni (Sh22.4 trilioni) kwa kipindi hicho ikilinganishwa na ilivyokuwa Oktoba 2021 kutokana na kuongezeka kwa thamani ya bidhaa zisizo za mazao na huduma.


Soma zaidi:


Ukuaji wa mauzo ya bidhaa zisizo asilia kwa kiasi kikubwa ulitokana na kuimarika kwa mauzo ya nguo, chuma, almasi, bidhaa za samaki na mbolea. 

Mauzo ya madini ya almasi nje ya nchi yaliongezeka kwa kiasi kikubwa hadi Dola za Marekani milioni 58.6 (Sh136.7 bilioni) kutoka Dola za Marekani milioni 3.8 (Sh8.8 bilioni) zilizorekodiwa katika kipindi kama hicho mwaka 2021.

Hali hiyo ilitokana na kurejeshwa kwa uzalishaji katika mgodi Williamson uliopo Mwadui mkoani Shinyanga baada ya kipindi cha matunzo na matengenezo.

Pia bidhaa asilia zenye thamani ya Dola za Marekani milioni 742.7 (Sh1.7 trilioni) ziliuzwa nje ya nchi katika mwaka unaoishia Oktoba 2022 yakiongezeka kutoka Dola za Marekani milioni 672.7 (Sh1.5 trilioni) katika kipindi kama hicho mwaka 2021. 

“Ufanisi huu ulichangiwa na ongezeko la mauzo ya korosho, tumbaku, pamba na mkonge,” imeeleza BoT. 

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV