Yaliyomo yamo “Samsung Unpacked 2023”

January 31, 2023 2:01 pm · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Matoleo matatu ya simu na kompyuta za “Book 3” kuachiliwa kesho
  • Zitatumia “processor” kubwa zaidi sokoni.
  • Toleo la Ultra kuwa na kamera ya MP 200.

Dar es Salaam. Bado una simu yako ya mwaka jana? Huenda matoleo mapya yanayotarajiwa kutangazwa kesho yakakupa mshawasha wa kujisasisha na simu mpya.

Kampuni ya kutengeneza vifaa vya kielektroniki ikiwemo simu, televisheni na vifaa vya nyumbani, Samsung, inatarajia kutangaza bidhaa mpya kesho (Februari 1, 2023) katika hafla ya mtandaoni itakayoanza saa tatu usiku. 

Bidhaa hizo zinazotarajiwa kutangazwa, ni mwendelezo wa matoleo ya Galaxy ambayo hutolewa na kampuni hiyo kila mwaka.

Kwa mwaka jana, Samsung iliingiza sokoni Samsung Galaxy S22 Ultra, Samsung Samsung Galaxy Watch4, Sumsung Galaxy TabS8 pamoja na Samsung Galaxy S 22 na S 22 Plus.

Kwa mwaka huu, haya ndiyo tunayo yatarajia

Simu tatu za kufungulia mwaka

Ni kawaida ya Samsung kufungua mwaka na simu tatu. Kwa mwaka huu, kutakuwa na Samsung Galaxy S23, Galaxy S23 Plus, na Galaxy S23 Ultra.

Simu hizo zinatarajiwa kuwa na uwezo wa kumbukumbu (memory) kuanzia jigabaiti 256 (GB). Uwezo ambao ni mkubwa kuliko simu shindani. Kwa simu nyingi zilizopo sasa, uwezo wa kumbukumbu wa chini zaidi ni GB 128.

“Prossesor” kubwa kuliko

Fahamu: Proccesssor ni kama akili ya simu yako. Kazi yake ni kuhuisha kila agizo (command) ambalo unaipatia simu yako. Hiyo inamaanisha, endapo processor ikiwa kubwa, uwezo na kasi ya simu kutekeleza maagizo ya mtumiaji wake ni mkubwa pia.

Kwa mujibu wa tovuti ya teknolojia ya Deccan Herald toleo la 23 linaingia sokoni na processor ya “Snapdragon 8 Gen 2” ambayo inatajwa kuwa yenye nguvu zaidi sokoni kwa sasa. Uzuri ni kuwa, teknolojia hiyo itatumika katika simu zote tatu.

Teknolojia hiyo inatarajiwa kumpatia mtumiaji matumizi rahisi ya simu, betri kutumika kwa muda mrefu zaidi na uwezo mzuri wa kung’amua picha.

Kamera za kumlingishia “Ex” wako

Yeye ana macho matatu au siyo? Na wewe yako yamewadia. 

Kamera za Samsung S22 zilikuwa poa lakini kamera za mwaka huu, wacha tuzingoje.

The Verge imeandika kuwa, kamera ya S23 Ultra inatarajiwa kuwa na Mega Pixel (MP) 200, sasisho kutoka MP 108 ya Galaxy S22 Ultra. S 23 Ultra inatarajiwa kuwa na kamera nne ambazo ni MP 12 za kamera ya mapana (ultrawide), MP 10 za kamera ya mbali (telephoto) na MP 10 za kamera nyingine ya “telephoto”.

Kati ya simu hizo, Galaxy S23 ni ndogo zaidi ikiwa na ukubwa wa inchi 6.1 ikifuatiwa na S23 Plus ambayo ina ukubwa wa inchi 6.6 huku S23 Ultra ikiwa na ukubwa wa inchi 6.8.

Pamoja na simu, Samsung inatarajia kutangaza toleo jipya la kompyuta zake ambazo ni Galaxy Book 3 and Book 3 Pro. 

Tovuti ya The Verge imeandika kuwa, huenda kukawa na “earbuds”, tableti na saa janja.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV