Jinsi ya kutengeneza picha kwa akili bandia mtandaoni

February 9, 2023 1:34 pm · Davis Matambo
Share
Tweet
Copy Link
  • Programu ya DALL-E 2 inaweza kuunda picha asili, halisi na sanaa kutokana na maelezo ya maandishi.
  •  Itawawezesha watu kujieleza kwa ubunifu.

Dar es Salaam. Unavutiwa na picha za mtandaoni? Na unapenda na wewe utengeneze kwa matumizi mbalimbali? Teknolojia iko kwa ajili yako. 

Programu tumishi ya DALL-E 2 inayotumia akili bandia imerahisisha zoezi hilo kwa kutumia njia rahisi ya uundaji wa picha mtandaoni kwa kuchakata maneno kutengeneza picha.

DALL·E 2 ni mfumo mpya wa akili bandia (AI) ambao unaweza kuunda picha na sanaa halisi kutokana na maelezo ya lugha asilia.

Programu hii inatumia uhusiano kati ya taswira na maandishi yanayotumiwa kuzielezea kupitia mchakato unaoitwa “diffusion” ambao huanza na muundo wa nukta nasibu na polepole kubadilisha muundo huo kuwa picha inapotambua vipengele mahususi vya picha hiyo.

Mfumo huu ulioundwa na kampuni ya OpenAI mnamo Januari 2021 kwa kutumia toleo  la GPT-3 lililorekebishwa kuunda picha, unawezesha kufanya uhariri kwenye picha zilizopigwa kutokana na maandishi ya lugha asilia. Pia  Inaweza kuongeza na kuondoa vipengele huku ikizingatia vivuli, uakisi na maumbo.

Jinsi ya kutumia DALL-E 2

Hatua ya 1. Ikiwa ni mtumiaji wa mara ya kwanza ingia kwenye wavuti ya OpenAI kusajili akaunti bure, pia unaweza kuingia kupitia Google au Microsoft. OpenAI itahitaji uthibitishaji wa mambo mawili, kwa hivyo weka simu yako karibu unapoanza mchakato huu.

Hatua ya 2: Baada ya kukamilisha hatua ya usajili OpenAI itafungua DALL-E 2 na kukueleza mchakato wa ulipaji au jinsi unavyoweza kuendelea kutumia huduma hii bure kwa muda.

Mtumiaji anapojisajili mara ya kwanza anapata ofa ya kutumia bure kwa mwezi wa kwanza, baada ya hapo atapata bure credit 15 pekee kila mwezi. Hata Hivyo watumiaji wanaweza kuongeza salio lao muda wowote kupitia dula la OpenAI kwa Tsh 35,100 na kupata credit 115 za kufanyia kazi. 

Hatua ya 3: Kwenye skrini ya DALL-E 2, utaona machaguo machache tofauti ili kuanza. Unaweza kuandika maelezo yako mwenyewe, kupakia picha ili akili bandia ibadilishe kulingana na maagizo yako, au uchague “surprise me” Nishangaze, ambapo maelezo yaliyoundwa kiotomatiki yatakuundia picha.

Ikiwa utaandika maelezo yako mwenyewe kumbuka, una kiwango kidogo tu cha salio, hivyo ni muhimu kuwa mwangalifu unapoandika maelezo ili kupata matokeo maalum unayokusudia.


Soma zaidi:


Hatua ya 4: Andika maelezo yako kwa taswira ya kibunifu au kisanii yenye urefu wa herufi 400 au pungufu, licha ya picha unaweza kuamuru kuunda michoro, sanaa za kidigitali au aina yoyote ya ubunifu mahususi unaopenda kujaribu. Chagua Tengeneza ukiwa tayari.

Hatua ya 5: Kwa kila ombi, DALL-E 2 itatoa picha kadhaa tofauti kwako kuchagua. Tafuta unayoipenda, na utumie vitufe vilivyo kwenye kona ya juu kulia ili kupendelea mwonekano au kupakua kwa muda huo.

Hatua ya 6: Ikiwa picha sio unayotaka, unaweza kujaribu kuchagua “Variations” Tofauti, ambapo teuzi mpya zitazalishwa kulingana na picha uliyochagua. Au unaweza kurudi nyuma na kujaribu kurekebisha kifungu chako cha maneno ili kupata matokeo tofauti.

Hatua ya 7: Wakati mwingine kubainisha nyakati tofauti na kubadilisha neno moja tofauti au mawili, kunaweza kuleta tofauti kubwa. Hivyo basi ni muhimu kufikiria jinsi unavyotaka picha ionekane na ujaribu kitu kipya ikiwa ni lazima ingawa matokeo yanaweza kuwa yasiyotarajiwa.

Unaweza kuuza picha ulizobuniKwa mujibu wa Sera ya Maudhui na Sheria na Masharti, unamiliki picha unazounda kwa kutumia DALL·E, ikijumuisha haki ya kuchapisha upya, na kuuza kama bidhaa – bila kujali kama picha ilitolewa kupitia mfumo usiolipishwa au unaolipiwa.

Enable Notifications OK No thanks