Benki ya Dunia: Tanzania kinara ukuaji uchumi Kusini mwa Jangwa la Sahara

February 13, 2023 3:17 pm · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Kuimarika kwa Sekta binafsi na kukua kwa  utalii vyatajwa kuwa sababu.
  • Mfumuko wa bei bado unawaumiza wananchi wa hali ya chini.

Dar es Salaam. Huenda unafuu wa maisha pamoja na upatikanaji wa huduma mbalimbali za kijamii ukaimarika nchini mara baada ya Benki ya Dunia kuripoti kuwa uchumi wa Tanzania unaimarika kwa kasi zaidi kuliko mataifa yote yaliyopo kusini mwa Jangwa la Sahara.

Benki hiyo katika ripoti yake ya hali ya uchumi wa Tanzania toleo la 18 ambayo imezinduliwa hii leo Februari 13, 2023 imeeleza kuwa baada ya kuathirika na janga la Uviko-19 kasi ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania ni ya kuridhisha ingawa inakabiliwa na vita ya Urusi na Ukraine.

“Hatua za kiuchumi zilizochukuliwa zimeifanya kasi ya ukuaji kuwa katika hali nzuri ingawa bado inakabiliwa na athari za vita inayoendelea ya Urusi na Ukraine, “ inasomeka sehemu ya ripoti hiyo.

Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, uchumi wa mataifa ya kusini mwa Jangwa la Sahara mwaka 2020  ulishuka kwa asilimia mbili huku waTanzania ukisalia palepale na kisha ukaongezeka kwa asilimia 4.3 mwaka 2021 na kuzidi wastani wa ukuaji kwa nchi hizo ambao ulikuwa kwa asilimia 4.2


Zinazohusiana


Ripoti hiyo imebainisha kwamba kasi ya ukuaji uchumi imekuwa kubwa zaidi katika miezi tisa ya mwanzo ya mwaka 2022 ambayo imechochewa na ukuaji wa sekta binafsi, kuimarika kwa sekta ya utalii, kukua kwa biashara pamoja na matumizi ya Serikali.

Kwa mujibu wa ofisi ya Taifa ya Takwimu NBS mwaka 2022 umerekodi kiwango kikibwa zaidi cha watalii tangu mlipuko wa janga la Uviko-19 utokee ambapo jumla ya watalii 1.45 milioni waliingia nchini ukilinganisha na watalii 922,692 walioingia nchini mwaka 2021.

Mfumuko wa bei bado tatizo

Licha ya mfumuko wa bei nchini Tanzania kuwa wa kiasi kwa mujibu wa viwango wa kikanda, benki hiyo imebainisha kuwa mfumuko wa bei uliochochewa na kupanda kwa bei ya mafuta na vyakula umesababisha hali ya maisha kuwa ngumu zaidi kwa watu wa hali ya chini.

Itakumbukwa kwa Februali mwaka huu NBS katika taarifa yao walibainisha kuwa kasi ya mfumuko wa bei muhimu za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Januari 2023 umeongezeka hadi asilimia 4.9 kutoka asilimia 4.8 kwa mwaka ulioishia Disemba 2022. 

Jambo lililochangiwa na kuongezeka kwa mfumuko wa bei kwa baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
31 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
31 May, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

Nukta TV

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

Nukta TV

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

Nukta TV