Zifahamu simu 5 zenye kasi zaidi ya mtandao wa 5G
- Ni pamoja na Galaxy Z Fold 4, IPhone 14 Pro Max na Google Pixel 7 Pro.
Dar es Salaam. Miaka ya hivi karibuni kampuni za simu duniani zinawekeza katika utengenezaji wa vifaa vyenye uwezo wa kutumia mtandao wa intaneti wenye kasi ya 5G.
Kampuni maarufu kwa uendeshaji wa programu ya upimaji wa kasi ya intaneti ya Ookla ya Marekani imetoa orodha ya chapa na simu janja zenye uwezo mkubwa wa 5G kwa 2022.
Simu ya hii ndiyo imetajwa kuwa na kasi zaidi ya intaneti duniani kwa sasa. Inatoa kasi bora zaidi ya upakuaji wa vitu mtandaoni ambapo megabaiti 147.25 (Mb) unaweza kupakua kwa sekunde moja ikiwa unatumia 5G.
Kasi yake ya wastani ya upakiaji wa 5G ni 13.95Mb kwa sekunde, na muda wa kusubiri ukiwa sekunde moja tu.
Simu hii inayotengenezwa na kampuni ya Google inashika nafasi ya pili kwa wastani wa kasi ya upakuaji ya 5G ya 137.11Mb kwa sekunde, kasi ya upakiaji ya Mb 15.53 kwa sekunde na muda wa kusubiri wa sekunde 1.
Simu ya Google Pixel 7 Pro ni miongoni mwa simu zenye kasi kubwa ya intaneti duniani kwa sasa. Picha | The Indian Express.
Kutoka kampuni ya Apple, simu hii imewekwa katika nafasi ya tatu kwa kutoa wastani wa kasi ya upakuaji wa 5G ya 133.84Mb kwa sekunde. Ukibahatika kuitumia utaweza kupakia kitu chenye ukubwa 15.39Mb mtandaoni kwa sekunde moja tu na muda wa kusubiri ukiwa milisekunde 54 yaani ndani ya sekunde moja tu.
Imeshika nafasi ya nne kwa kasi ya upakuaji ya 130.14Mb kwa sekunde, huku kasi ya upakiaji ikiwa 14.41Mb kwa sekunde, na muda wa kusubiri chini ya dakika moja.
Simu hii kutoka kampuni ya Samsung yenye makao makuu nchini Korea Kusini imeshika nafasi ya tano kwa kuwa na kasi ya wastani ya upakuaji wa 124.83Mb kwa sekunde.
Kasi ya upakiaji ya 12.6Mb kwa sekunde, huku muda wa kusubiri ukiwa milisekunde 57 kwenye mitandao ya 5G.
Hadi sasa, simu zenye uwezo wa 5G kutoka Samsung ndizo zinatoa kasi kubwa zaidi ya kupakua na kupakia nchini na kuizidi Apple kwa kutoa wastani wa kasi ya upakiaji wa 79.3Mb kwa sekunde kwenye simu zake zote.Simu za Samsung Galaxy zina kasi ya wastani ya upakiaji ya karibu 9.88 Mb kwa sekunde, wakati muda wa kusubiri ukiwa milisekunde 58.
Kwa kulinganisha, kasi ya wastani ya upakuaji wa 5G kwenye iPhones ni 72.62Mb kwa sekunde, na wastani wa kasi ya upakiaji wa 5G ni 8.69Mb kwa sekunde na muda wa kusubiri wa wastani wa chini ya dakika moja.Simu za Samsung Galaxy S23, Galaxy S23+ na Galaxy S23 Ultra, zitakazozinduliwa Februari 1, 2023, zinatajwa kuwa na kasi ya upakuaji na upakiaji wa haraka zaidi kwenye mitandao ya 5G.
Zinazohusiana
- Jinsi ya kubaini kamera zilizofichwa kwenye nyumba ya kupanga, chumba cha hoteli
- Namna ya kupima ugonjwa wa rimoti kwa kamera ya simu
Kwa upande wa ripoti za vichakataji (Chipset) kampuni ya Ookla imeorodhesha Snapdragon 8+ Gen 1 kama chipset ya haraka zaidi, ikiwa na kasi ya wastani ya upakuaji ya megabaiti 141.49 kwa sekunde.
Tensor G2 yenye modemu ya Samsung 5G inashika nafasi ya pili ikiwa na wastani wa kasi ya upakuaji wa 134.87Mb kwa sekunde. Snapdragon 8 Gen 1 na Snapdragon 888 zinashika nafasi ya nne na tano.
Kampuni ya T-Mobile imeongoza nafasi ya mtoa huduma wa mtandao wa simu za mkononi mwenye kasi zaidi nchini Marekani mnamo robo ya mwisho ya 2022, ikiwa na kasi ya wastani ya upakuaji ya megabaiti 216.56 kwa sekunde na muda wa kusubiri wa milisekunde 53.
Verizon inashika nafasi ya pili kwa kasi ya upakuaji ya megabaiti 127.95 kwa sekunde na muda wa kusubiri wa wastani wa chini ya dakika. AT&T imeshika nafasi ya tatu ikiwa na kasi ya upakuaji ya wastani ya 5G ya megabaiti 83.59 kwa sekunde na muda wa kusubiri wa chini ya dakika.