Tanzania iko tayari kuilisha dunia?

March 17, 2023 2:21 pm · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Uzalishaji wa chakula waimarika nchini.
  • Uuzaji wa mazao nje ya nchi waongezeka kila mwaka. 

Dar es Salaam.  Huenda siku zijazo Tanzania ikaongeza wigo wa kuuza mazao na kulisha nchi mbalimbali duniani baada ya sekta ya kilimo kuimarika nchini na kuongezeka kwa mauzo ya chakula nje ya nchi. 

Kwa mujibu wa takwimu kutoka Benki ya Tanzania (BoT) na Wizara ya Kilimo, Tanzania imekuwa ikiongeza mauzo ya nje ya chakula mwaka hadi mwaka, huku chakula hicho kikiuzwa nchi za Afrika Mashariki, Kusini mwa Afrika, Pembe ya Afrika (Horn of Africa) na sehemu nyingine duniani.

Takwimu hizo zinaonesha kuwa Tanzania iliuza mbogamboga zenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 1.01 (Sh2.4 trilioni) katika kipindi cha miaka mitano kati ya mwaka 2018 hadi 2022.

Tanzania pia iliuza mazao ya nafaka (zaidi mchele na mahindi) yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 999 (Sh2.3 trilioni) katika kipindi hicho cha miaka mitano iliyopita.

Mauzo ya nje ya nchi ya samaki na bidhaa za samaki yalifikia Dola za Marekani milioni 800 sawa na Sh1.9 trilioni, wakati matunda yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 71.4 sawa na Sh170 bilioni kati ya 2018 na 2022.


Soma zaidi:


Uzalishaji nao tuko vizuri

Tanzania ni miongoni mwa wazalishaji wakubwa watano wa mchele barani Afrika na ndiyo mzalishaji mkubwa zaidi wa mchele Afrika Mashariki.

Katika msimu wa 2020/21, Tanzania ilizalisha tani milioni 1.85 za mchele, wakati mahitaji ya nchi kwa mwaka ni takribani tani milioni 1. Hiyo ina maana kuwa mchele wa ziada ulikua tani 850,000.

Katika msimu huo huo, Wizara ya Kilimo imeeleza kuwa Tanzania ilizalisha tani milioni 6.5 za mahindi, ukilinganisha na nahitaji ya Taifa ya tani milioni 6 kwa mwaka.

Mafanikio hayo yamepatikana wakati Rais Samia Suluhu Hassan leo akizindua maandalizi ya mkutano mkubwa wa Kilimo wa Afrika (Africa Food Systems Forum) ambao unatarajiwa kufanyika Tanzania Septemba 5 hadi 8, mwaka huu.

Uzinduzi huo umefanyika Ikulu, Dar es Salaam ambapo, Rais amewataka Watanzania kutumia mkutano huo kama fursa ya kutengeneza ajira na kutafuta masoko ya bidhaa zinazozalisha nchi hasa za kilimo.

Tangu aingie madarakani Machi 2021, Rais Samia ameongeza bajeti ya Serikali kwenye kilimo maradufu kwa viwango vya juu tangu Tanzania ipate. 

Mafanikio katika sekta ya kilimo nchini yametokana uwekezaji mkubwa na wa muda mfupi uliofanywa na Serikali ya Rais Samia ikiwemo kutoa ruzuku ya mbegu, rmbolea, uzalishaji mbegu na kilimo cha umwagiliaji.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV