Dk Mabula awaonya wanaobadili matumizi ya hati za ardhi

April 19, 2023 12:52 pm · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula (Kulia) akigawa hati za ardhi kwa wakazi wa Halmashauri ya Ilemela mkoani Mwanza. Picha | Mariam John. 


  • Asema zinaharibu muonekano wa miji na mipango yake.
  • Awaonya wenye tabia hiyo kuwa watachukuliwa hatua. 

Mwanza. Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula amewataka wananchi wanaokabidhiwa hati miliki za ardhi kuhakikisha wanazingatia masharti yaliyopo kwenye hati hizo na kufuata mipango kabambe ya maeneo husika ikiwemo kutobadili matumizi ya hati hizo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi hati 570 kwa wakazi wa kata ya Shibula  wilayani Ilemela katika Mkoa wa Mwanza, Waziri Mabula amesema ipo tabia ya baadhi ya wananchi wanaaomba hati hizo kubadilisha matumizi, kitu ambacho hakikubaliki.

“Huwezi kupata hati leo, kesho unaenda kubadili matumizi mwisho wake miji inaonekana haina maana  na haipendezi na sisi tunataka jiji la Mwanza na Ilemela iwe ya  mfano,” amesema Dk Mabula.

Waziri huyo amewetaka watendaji wa sekta ya ardhi na uongozi wa Serikali wasimamie matumizi sahihi ya hati hizo na kuzuia kila namna ya kubadili kwa matumizi.

Hata hivyo, Waziri huyo ameshtushwa na idadi ndogo ya wamiliki waliojitokeza kuchukua hati ambao ni 50 kati 570 wenye hati hizo.

Amewataka wamiliki wa ardhi walioshindwa kuchukua hati kuandaliwa utaratibu maalumu wa kupatiwa hati hizo na kuitaka idara ya ardhi katika Halmashauri ya  Ilemela kwa kushirikiana na ofisi ya Kamishina wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Mwanza kuchagua sehemu moja na kutumia wiki mbili kutoa hati hizo kwa wahusika ili ziishe na kuendelea mchakato wa hati nyingine. 

“Watu tuna tabia ya kulalamikia hati hazitoki hapa tuna hati 570 lakini waliojitokeza ni 50 tu wengine wako wapi? Ni kitu ambacho  hakieleweki hati zinaandaliwa lakini hawaji kuchukua naomba zile zinazobaki muangalie namna mtakavyotoa,” amesema Dk Mabula.

Hezroni Simon ni mkazi wa kata hiyo amesema ana furaha kwa kuwa amekuwa akifuatilia hati hiyo kwa muda wa miezi sita sasa lakini hatimaye leo ameipata.

“Nimekuwa nikifuatilia hati kwa muda mrefu lakini leo nimefanikiwa kupata hati yangu ambayo itanisaidia katika kulinda eneo langu lakini ni mtaji ambapo naweza kuitumia katika kupata mikopo kwenye taasisi za kibenki,” amesema Simon. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
8 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
8 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Ulinzi waimarishwa Dar, maduka yachelewa kufunguliwa

Ulinzi waimarishwa Dar, maduka yachelewa kufunguliwa

Nukta TV

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV