Miongozo mipya elimu maalum kuongeza ujumuishi Tanzania

September 12, 2023 12:17 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni pamoja na elimu ya nyumbani na ziara za nyumbani.
  • Itaondoa changamoto zinazowakabili wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Dar es Salaam. Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, profesa Adolf Mkenda amezindua miongozo mipya ya elimu inayotarajiwa kuongeza ujumuishi wa elimu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum waliopo nchini.

Kwa muda mrefu Tanzania haikuwa na muongozo maalum wa kufikisha elimu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum hivyo hatua hiyo inatarajiwa kuleta ahueni kwa wadau wa elimu ikiwemo wazazi, walimu, watoa huduma za kielimu, na  wakuza mitaala.

Waziri Mkenda aliyekuwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa miongozo hiyo leo Septemba 12, 2023, amewaambia washiriki kuwa itaondoa changamoto zinazowakabili wanafunzi wenye mahitaji maalum.

“Kila muongozo umeandaliwa kwa namna itakayowezesha kuboresha mazingira ya kielimu kwa kuzingatia mahitaji mahususi ya kila mwanafunzi,” amesema Waziri Mkenda.

Miongozo hiyo ni pamoja na ule wa  shule za nyumbani, ziara za majumbani, ubainishi wanafunzi wenye mahitaji maalum, uanzishwaji na uendeshaji shule au vyuo vya wanafunzi wenye mahitaji maalum na jumuishi.

Kwa mujibu wa Rais Samia Suluhu Hassan, aliyekuwa akizungumza  katika shule ya Sekondari Benjamin Machi 7, 2023, mpaka mwaka 2021 Tanzania ilikuwa na jumla ya watoto 28,968 wenye mahitaji maalum.


Soma zaidi


Itawezesha ufuatiliaji wa karibu

Marita Shayo, Afisa Elimu Maalum kutoka Same mkoani Kilimanjaro, aliyekuwa akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa miongozo hiyo amebainisha kuwa  ziara za majumbani zitakazofanyika kila ijumaa zitawezesha ufuatiliaji wa karibu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.

“Tunapoenda kuwatembelea nyumbani tunafanya ulinganifu kwa yale waliyojifunza shuleni je yanaendelezwa  kule nyumbani…huu ndio muda muafaka wa kuangalia changamoto za kiafya na kushauriana na wazazi jinsi ya kufanya,”  Shayo.

Muongozo huo wa ziara ya nyumbani utatoa nafasi kwa maafisa elimu maalum kutazama maendeleo ya mtoto pamoja na utolewaji wa ushauri wa kisaikolojia kwa wazazi na walezi wa watoto hao.

Mkurugenzi wa Elimu kwa Wenye Uhitaji Maalum Magreth Matonya, akizungumza na wahudhuriaji wa hafla ya uzinduzi wa miongozo maalum ya elimu jumuishi.Picha|Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia/Twitter.

Kurahisisha ugunduzi wa vipawa maalumu

Aidha, Mkurugenzi wa Elimu kwa Wenye Uhitaji Maalum Magreth Matonya, ameongeza kuwa  muongozo wa ubainishaji na upimaji wa watoto wenye vipawa maalum utasaidia kutambua wanafunzi wenye vipaji maalum.

Kwa mujibu wa Matonya uwezo wa wanafunzi wenye vipaji maalum  hauwaruhusu kukaa darasani na kujifunza sawa na wanafunzi wengine.

Mwongozo huo unatarajia kutumika zaidi wakati wa utekelezaji wa Sera  mpya ya elimu itakayotambua uwepo wa wanafunzi na shule za vipaji maalum.

“Utatusaidia kubaini kama ni mkondo wa taaluma, au ni mkondo wa amali au ni mkondo mwingine wa vipawa mbalimbali ambavyo watoto wanavyo,” amebainisha Matonya.

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV