Rais Samia : Simamieni haki kuimarisha imani ya mahakama Tanzania

September 14, 2023 12:35 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Asisitiza kufanya kazi kwa maadili kuchochea upatikanaji wa haki
  • Mahakimu, majaji wasio waadilifu kuchukuliwa hatua

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amewataka majaji kusimamia haki ili kujenga imani ya mahakama kwa wananchi na kuongeza ufanisi katika shughuli za mhimili huo muhimu.

Rais Samia aliyekuwa akizungumza leo Septemba 14, 2023 wakati akiwaapisha viongozi aliowateua Ikulu jijini Dar es Salaam, amebainisha kuwa wateule hao watasaidia kupunguza mlundikano wa kesi na kuongeza ufanisi katika shughuli za mahakama.

“Ni imani yetu kuwa mlioteuliwa mtaenda kufanya kazi kwa jitihada zote ili mabadilko tunayozungumza tukayaone…tunaomba muongeze nguvu ili mkafanye vizuri na haki ipatikane mapema,” amesema Rais Samia.


Soma zaidi


Viongozi walioapa leo ni pamoja na majaji wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu, ikiwa ni sehemu ya  utekelezaji wa mapendekezo ya tume ya haki jinai iliyoshauri kuimarisha uwezo wa mahakama katika teknolojia, kuboresha majengo na rasilimali watu.

Tangu Rais Samia aingie madarakani mwezi Machi mwaka 2021, ameteua majaji wa mahakama kuu 63, na kufanya Tanzania iwe na jumla ya majaji 105, idadi  inayotajwa kuiweka Tanzania kwenye nafasi nzuri ya kutoa haki kwa wananchi.

Wasio na nidhamu watahadharishwa

Kufuatia kuwepo kwa vitendo vya uvunjifu wa maadili unaofanywa na majaji na mahakimu katika mahakama, Serikali kupitia Mahakama Kuu imeanzisha tume inayyochunguza mwenendo wa maadili ya viongozi hao.

Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma amebainisha kuwa kuanzia mwaka mwaka 2015 hadi 2019 jumla ya mashauri 99 ya uvunjifu wa maadili yalikusanywa ambapo 33 kati yao walifukuzwa kazi huku 38 wakistaafishwa.

“Waliofukuzwa kazi  na kustaafishwa ni asilimia 71…kwa hiyo majaji msiingie katika anga ya tume katika masuala ya nidhamu,” amesema Profesa Juma.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
25 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
25 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

Nukta TV

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV