Maumivu ushuru wa mawigi kuanza leo

July 1, 2022 7:56 am · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni wa asilimia 35 kwenye nywele bandia zinazotoka nje ya nchi.
  • Watumiaji wasema itaongeza gharama za maisha.

Dar es salaam. Tanzania inaanza kutekeleza makubaliano ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ya kutoza ushuru wa asilimia 35 katika nywele bandia (mawigi) yanayoagizwa nje ya nchi huku ukiacha maumivu kwa wafanyabiashara na watumiaji wa bidhaa hiyo. 

Ushuru huo ambao umepanda kutoka asilimia 25 ya awali ulipitishwa katika Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2022/23 

Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Dk Mwigulu Nchemba wakati anawasilisha pendekezo hilo Bungeni Juni 16 mwaka huu alisema ushuru huo makubaliano ya  EAC ambayo inaundwa na nchi saba ikiwemo Tanzania.

“Nchi wanachama  za Jumuiya ya Afrika Mashariki zimekubaliana kuongeza ushuru wa forodha kutoka asilimia 25 mpaka asilimia 35,  kutoka kwenye nywele bandia,” alieleza Waziri Nchemba na kubainisha kuwa hatua hiyo itaongeza mapato ya Serikali.

Waziri huyo alisema lengo ni kulinda na kuviongezea uwezo viwanda vya ndani kuzalisha na kujipatia soko la uhakika la bidhaa hiyo kutoka kwa watumiaji. 

Hata hivyo, ushuru kwa bidhaa hiyo inayozalishwa na viwanda vya ndani haujabadilika imebaki asilimia 10 ya awali ambayo ilianza kutumika mwaka 2019/20.

Baadhi ya watumiaji wa mawigi waliambia Nukta Habari (www.nukta.co.tz) kuwa amesema kupandisha ushuru ni kuwaumiza zaidi Wananchi kwani bidhaa nyingine zimekwisha panda bei. 

“Kila mtu ana uchaguzi wa kutumia wigi analopenda, wengine wanapenda yanayotoka nje ya nchi, hivyo kupandisha ushuru inaweza kuwanyima haki ya kuchagua,” alisema Getrude John mkazi wa Bunju jijini Dar es salaam.

Wakati waagizaji wa nje  watalazimika kutoboa zaidi mifuko yao,kutokana na ongezeko la tozo huenda itakuwa kicheko kwa wazalishaji wa ndani wa bidhaa hiyo kwa sababu watafaidika na wateja ambao wataachana na mawigi ya nje, hivyo kuwaongezea faida.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Nukta TV

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Nukta TV