Elimu bora kuwanasua watoto wenye ulemavu Mwanza

February 24, 2024 10:27 am · Abdushakur
Share
Tweet
Copy Link
  • Wadau wasema mkoa wa Mwanza bado unahamasa ndogo ya kuwapeleka watoto wenye ulemavu shuleni.
  • Baadhi ya shule yaanzisha vitengo maalum vya kuhudumia walemavu.

Mwanza. Miezi miwili baada ya kuanza kwa muhula wa masomo kwa mwaka 2024, wadau wa elimu jijini Mwanza wametoa rai kwa jamii kuachana na mila potofu zinazozuia watoto wenye ulemavu  kupelekwa shule.

Kwa muda mrefu sasa jiji hilo limekuwa likikabliwa na mila potofu na tamaduni zinazowafanya baadhi ya wazazi wenye watoto walemavu kuwafungia ndani wakiamini kundi hilo haliwezi kupata elimu, jambo ambalo si kweli na linarudisha nyuma maisha ya watu wenye ulemavu.  

Wadau wa elimu na watetezu wa haki za binadamu wameiambia Nukta Habari kuwa licha ya Serikali kuboresha miundombinu ya elimu kwa watoto wenye ulemavu, bado kuna hamasa ndogo kwa wazazi na walezi kuwapeleka  watoto hao shuleni.

“Kila mtoto ana haki ya kwenda shule awe mlemavu, kiziwi ama vyovyote vile, inabidi kuhamasisha ili watoto hao wapate elimu,” amesema Shamimu Said mdau wa elimu na mkazi wa Wilaya ya Nyamagana jijini humo.

Shamimu anaeleza kuwa wakati wakiendelea na juhudi za kubadilisha jamii hiyo, ni vyema kujikita zaidi katika kutoa elimu kwa wazazi na walezi wa watoto hao ili kuwapatia haki yao ya msingi ya kupata elimu.

Baadhi wanaonya kuwa ni hatari kupuuza umuhimu wa elimu katika jamii ili kuhakikisha kila mtoto anapata elimu stahiki.

Mdau wa elimu jijini humo Tariki Doto anasema kama wadau hao wakipuuzia suala la elimu kutakuwa na idadi kubwa ya watoto wenye mahitaji maalumu watakaokosa haki ya msingi ya kupata elimu.

Watoto hao wenye ulemavu mkoani Mwanza ni miongoni mwa watoto milioni 240 ambao Shirika la Kimataifa la Elimu (Unesco) linawataja kuwa na ulemavu huku nusu yao wakikosa nafasi ya kupata elimu kutokana na sababu mbalimbali  ikiwemo kukosekana kwa mazingira wezeshi.

“Kwa sababu ya ukosefu wa elimu bora na mjumuisho, watoto wenye ulemavu wananyimwa fursa nyingi. Watu wengi bado wanaamini kuwa kujumuisha watoto wenye ulemavu katika madarasa ya kawaida ni changamoto sana kwa hiyo hawana ari kubwa ya kukuza elimu jumuishi,” imesema Unesco.


Soma zaidi: Elimu ya Veta inavyowainua walemavu wa akili Tanzania


Hali ilivyo shuleni

Wakati wadau wa elimu wakichagiza kuongeza idadi ya watoto wenye ulemavu shuleni, baadhi ya shule mkoani humo zimeanzisha vitengo maalum vya kuhudumia watoto hao ili kuongeza ushiriki wao katika elimu.

Shule ya Msingi Nyamalango iliyopo kata ya Luchelele wilayani Nyamagana jijini humo ni miongoni mwa shule zilizoanzisha vitengo maalum kwa ajili ya kuwasaidia watoto hao miaka takriban minne iliyopita. 

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Elumence Filbert, ameiambia Nukta habari kuwa kitengo cha elimu maalumu kwenye shule yake kilianzishwa mwaka 2020 kikiwa na wanafunzi 15, idadi iliyooongezeka hadi kufikia wanafunzi 75 mwaka jana.

“Jamii inabidi ifike hatua maneno mabaya wanayotoa kwa watoto wenye ulemavu tofauti wayaache, kwani yanashusha molari ya wanafunzi kujifunza, pia  wazazi na walezi kuona aibu kuwaleta watoto wao wapate elimu” ameongeza mwalimu Filbert.

Mbali na kuwajali watoto hao kwa kutumia lugha ya staha, Filbert anaishauri Serikali kuongeza kasi ya kuajiri walimu wa mahitaji maalum ili kupunguza uhaba uliopo kwa sasa na kuwapa hamasa wanafunzi hao kujifunza. 

Serikali yajifua kuwezesha wenye ulemavu kupata elimu

Serikali inaeleza kuwa ili kuhakikisha upatikanaji a elimu sawa kwa wote, wametekeleza kampeni mbalimbali za utoaji wa elimu kwa jamii juu ya elimu sawa kwa wote.

Allan Said, Afisa Elimu wa Halmashauri ya jiji la Mwanza amebainisha kuwa wamahamasisha wazazi na walezi ambao wana watoto wenye mahitaji maalum, wawapeleke shule ili kutoa haki sawa ya kupata elimu bora kwa kila mtu.

“Watu wajitoe wasione aibu, bahati nzuri wenyewe hawasumbuliwi (wanafunzi wenye mahitaji maalum),’’ amesema Said, na kutoa rai kwa jamii kuwaandikisha watoto hao katika shule mbalimbali zenye vitengo vya elimu maalumu, ili kuimarisha misingi ya utoaji elimu bora.

Wakati hayo yakiendelea jijini Mwanza, Serikali inajipanga kuongeza elimu na uboreshwaji wa miundombinu kuwezesha watoto wenye elimu kupata elimu bora.

Waziri wa  Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda, aliyekuwa akiwasilisha Bungeni bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka wa fedha 2023/24 katika wizara yake amesema Serikali imeendelea kuboresha miundombinu na vifaa mbalimbali inayowawezesha wanafunzi wenye ulemavu kupata elimu.

Miongoni mwa vifaa hivyo ni pamoja na vitimwendo 253 kwa wanafunzi wa shule za msingi 200 na sekondari 53 na vifaa saidizi vya kuongeza usikivu (hearing aids) 100 kwa wanafunzi wa elimu ya Msingi 30 na Vyuo Vikuu 70 

Vilevile, imekamilisha ujenzi na kuzindua Shule ya Msingi Jumuishi ya mfano ya Lukuledi iliyopo katika halmashauri ya Masasi na Shule ya Sekondari Patandi iliyopo halmashauri ya Wilaya ya Meru zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 480 kila moja.

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa kiwango cha biashara kati ya Tanzania na Sin

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa kiwango cha biashara kati ya Tanzania na Sin

Nukta TV

Mizinga ya heshima, Rais Samia akimpokea Rais wa Singapore, Ikulu Dar es Salaam

Mizinga ya heshima, Rais Samia akimpokea Rais wa Singapore, Ikulu Dar es Salaam

Nukta TV

Mikakati ya Serikali kuhakikisha walimu wa VETA wanapata ajira na mikopo

Mikakati ya Serikali kuhakikisha walimu wa VETA wanapata ajira na mikopo

Nukta TV