Guterres: Mfungo wa Ramadhan umalize mgawanyiko na kusaidia wahitaji

March 10, 2024 6:12 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ramadhan inatarajiwa kuanza Machi 12 mwaka huu.
  • Guterres ahimiza amani, upendo na mshikamano.

Dar es Salaam. Ikiwa zimebaki siku chache kwa waumini wa dini ya kiislamu kuanza mfungo wa Ramadhan, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Antonio Guterres amesema mfungo wa Ramadhan utumike kumaliza mgawanyiko na kusaidia wahitaji.

Mfungo wa Ramadhan ni miongoni mwa nguzo tano za uislamu ambapo kila mwaka waumini wa dini ya kiislamu hufunga kwa masaa 12 kwa muda wa siku 30 ambazo huhitimishwa kwa shamra shamra za sikukuu ya iddi.

Kwa mujibu wa Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu (Bakwata) Nuhu Jabir Mruma, mfungo wa mwaka huu nchiini Tanzania unatarajia kuanza Jumanne ya Machi 12, kutegemea  na kuandama kwa mwezi na utamalizika Aprili 10 au 11.


Soma zaidi:Mambo muhimu ya kuzingatia katika mfungo wa Ramadhan


Katika salamu zake kwa waumini wa dini ya kiislamu alizozitoa kwa njia ya video Machi 9, 2024 Guterres amesema kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhan kitumike kumaliza migawanyikona kuwasaidia wahitaji hususan katika nchi zenye vita na machafuko.

“Tuhamasike kumaliza mgawanyiko, kuwasaidia wenye uhitaji na kufanya kazi kwa pamoja kwa usalama na utu kwa kila mwanadamu,” amesema Gutteres.

Wakati baadhi ya nchi zikitarajia kuanza mfungo kwa amani, Guterres amesema bado kuna baadhi ya nchi zenye misingi ya kiislamu zitaingia katika kipindi mfungo zikiwa na mapigano na ukosefu mkubwa wa amani ikiwemo Afghanistan, Sahel,Syria na nchi nyingine za Afrika. 

Aidha kiongozi huyo amezitaka nchi zote duniani kuendeleza upendo na amani ambayo itasaidia kutengeneza dunia yenye haki na usawa utakaochochea maendeleo.

“Mwezi mtukufu ulete amani, na utuongoze kuelekea katika dunia yenye usawa na haki,” ameongea Guterres.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV