Chanjo ya Uviko-19 inapatikana katika vituo hivi Singida
Dar es Salaam. Kama uko katika Mkoa wa Singida iwe mjini au vijijini na una sifa za kupata chanjo ya Corona, Serikali imeweka vituo 21 katika Halmashauri saba za mkoa huo ili kutoa fursa kwa watu kuchanjwa.
Nenda kachanje ili uwe salama. Kumbuka chanjo husaidia kumkinga mtu na maambukizi ya ugonjwa wa Uviko-19. Kwa sasa, Tanzania inatumia chanjo aina ya Johnson & Johnson ambayo mtu anayechanjwa anapatiwa dozi moja tu.
