Accra kuwa mji mkuu wa dunia wa vitabu mwaka 2023

September 23, 2021 5:33 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Inakuwa jiji la 23 kupata hadhi hiyo tangu kuanzishwa kwa tukio hilo mwaka 2001.
  • Ghana inaamini vitabu vinaweza kuleta mabadiliko ya kitamaduni na utajiri wa nchi hiyo.

Dar es Salaam. Mji mkuu wa Ghana, Accra umetangazwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco) kuwa mji mkuu wa dunia wa vitabu kwa mwaka 2023.

Accra inakuwa jiji la 23 kupata hadhi hiyo tangu kuanzishwa kwa tukio hilo mwaka 2001. Miji mingine ya Afrika iliyowahi kupata hadhi hiyo ni Port Harcourt nchini Nigeria mwaka 2014 na Conakry Guinea mwaka 2017.

​Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Audrey Azoulay amesema kuwa hatua hiyo inazingatia tathmini ya kamati ya ushauri ya miji ya vitabu ya dunia baada ya kupitia andiko la Accra la kupanua wigo wa usomaji vitabu.

Mpango wa Ghana unatambua jinsi vitabu vinavyoweza kuleta mabadiliko ya kitamaduni na utajiri wa nchi hiyo kupitia watoto na vijana na hivyo kujenga kizazi kijacho chenye stadi thabiti.

Unesco imesema watakaojumuishwa kwenye mpango huo ni makundi yaliyo pembezoni yenye kiwango cha juu cha kutokujua kusoma na kuandika wakiwemo wanawake, vijana, wahamiaji, watoto wanaozurura mitaani na watu wenye ulemavu.

Sherehe zitaanza Aprili  23mwaka 2023 ambayo ni siku ya vitabu na hakimiliki duniani.

Mkakati wa utekelezaji unajumuisha kusambaza vitabu vya kusoma ili kujenga tabia ya kusoma vitabu ambapo pia sekta ya uchapishaji vitabu nayo inapatiwa hamasa.

Accra inatumia mbinu mbalimbali za kuhamasisha kusoma kwa kuanzisha pia maktaba tembezi sambamba na kufanyika kwa warsha za kuhamasisha uandishi wa vitabu kwa lugha mbalimbali za Ghana.

Andiko la Ghana kuweza kupata hadhi pia liligusia pia uhuru wa mtu kupata taarifa ikiwa ni kuelekea siku ya uhuru wa vyombo vya Habari mwaka 2023.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV