“Only One King” ya Alikiba ilivyokusanya nguli wa muziki Afrika

October 8, 2021 11:33 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Amewashirikisha wasanii nane kutoka Nigeria, Kenya, Ghana na Afrika Kusini.
  • Albamu yake ina jumla ya nyimbo 16 zikiwemo zilizokuwa zimeshaanza kusikika.
  • Wakali wengine kutoka lebo ya King’s Music, nao ndani.

Dar es Salaam. Kama bado haujafikiwa hata na muziki mmoja kutoka kwa msanii wa Bongo Fleva, Alikiba basi unahitaji kujitafutia uraia mwingine kwani albamu hii imefika kila kona.

Natania tu! Tanzania ni yetu sote.

Lakini kama bado huenda ukapata sababu baada ya kuona orodha ya nguli wa muziki barani Afrika walioambatana na Kiba kwenye albamu yake mpya.

Unaweza kuwa umesikia nyimbo baadhi ambazo zilikuwa zimetoka tangu awali ikiwemo Salute aliyoshirikiana na Rudeboy wa Nigeria ambayo hadi sasa imetazamwa na watu zaidi ya milioni 5.6 pamoja na Jelous aliyoimba na Mayorkun wa Nigeria ambayo imetazamwa na watu zaidi ya milioni 8 katikia mtandao wa YuTube.

Mwenendo wa usikilizwaji wa “Only One King” hadi Oktoba08, 2021 kwenye Boomplay. Picha| Rodgers George.

Mafanikio tangu itoke

Albamu ya “Only One King” ambayo kwa Kiswahili tafsiri yake ni Mfalme Mmoja Tu hadi sasa inapatikana kwenye majukwaa mbalimbali ya usikiliza muziki ikiwemo Boomplay, Deezer, Spotify, Youtube na Apple Music.

Kwa Boomplay, hadi sasa Kiba amejizolea wasikilizaji 732,200 wa albamu yake huku nyimbo zake zikiingia kwenye vipengele mbalimbali.

Wimbo wa Oya Oya unashika nafasi ya 18 kwenye orodha ya nyimbo bora 100 kwa Tanzania katika jukwaa la Boomplay ikiwa imepanda kutoka nafasi nje ya 100 huku “Jelous” ikishika nafasi ya 51 kwenye orodha ya nyimbo 100 bora kwa Afrika, ikishuka kutoka namba 5.

Kwa upande wa Youtube Charts, Oya Oya ina “trend” kwenye mtandao huo ikifuatiwa na Bwana Mdogo aliyoshirikiana na Patoranking. Jux na sina neno ameshika nafasi ya tatu na kuiacha nafasi ya nne Alikiba ikikamatwa na kibao cha Niteke ambacho ameshirikiana na Blaq Diamond.


Nguli Wa Muziki Afrika walioingia kwenye “Only One King”

Mbali na Watanzania Tommy Flavour, K2ga na Abdu kiba wa Kings Music, Alikiba ameshirikisha wasanii 8 wakali barani afrika. 

Katika albamu hiyo Alikiba ameimba na Rudeboy, Mayorkun na  Patoranking, wasanii kutoka Nigeria, Sarkodie (Ghana), Nyashiski, Khaligraph Jones na Sauti Sol (Kenya) pamoja na Blaq Diamond, nguli wa miondoko ya Afro Pop kutoka Afrika Kusini. 

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW